Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 9:57 am

NEWS: NCHI ZA UHISPANIA NA ITALIA ZAOMBA MSAADA KUIKABILI CORONA

Nchi za Uhispania na Italia ambazo kimsingi ndio zilizoathirika zaidi na vifo vinavyotokana na Virusi vya Corona zimezitaka nchi nyingine za bara Ulaya kuzisaidia wakati ambapo idadi ya maambukizi ya virusi vya corona ikiendelea kuongezeka katika nchi zao.

ICU patients with coronavirus and pneumonia treated in Wuhan ...

Idadi ya vifo vinavyotokana na Corona nchini Italia imefikia 10,779, huku idadi ya kesi juu ya watu walioambukizwa ugonjwa huo wakifikia 97,689. huku wenzao wa Uhispania idadi ya vifo vikifikia 6,808 na kesi za corona 80,110.

Ufaransa imesema mustakabali wa jumuiya ya Ulaya unategemea jinsi nchi wanachama zinavyopambana na mlipuko wa virusi vya corona hasa baada ya wajumbe wa jumuiya hiyo kushindwa wiki iliyopita kufikia makubaliano juu ya hatua za kuunusuru uchumi uliotetereka kutokana na janga la virusi vya corona.

Corona Symbolbild Europa Spanien (Getty Images/J. Soriano)

Umoja wa Ulaya unakabiliwa na mtihani mzito tangu kuzuka na kuendelea kuenea kwa virusi vya corona, mtihani huu unafuatia migogoro ya hivi karibuni iliyoitikisa jumuiya hiyo kama suala la Brexit, mgogoro wa wahamiaji wa 2015-2016 na mgogoro wa madeni katika eneo zima la nchi zinazotumia sarafu ya euro.

Waziri wa Ufaransa anayeshughulikia masuala ya Ulaya Amelie de Montchalin amesema uchumi wa nchi kama Ujerumani na Uholanzi hauwezi kuimarika ikiwa nchi nyingine za Ulaya zitabaki nyuma na ameongeza kusema kwamba vyama vya mrengo mkali wa kulia vitaibuka washindi ikiwa viongozi wa Umoja wa Ulaya watashindwa kufanya kazi pamoja wakati huu wa janga kubwa.

De Montchalin ametoa mfano uamuzi wa Ujerumani na nchi nyingine za Ulaya wa kuwachukua wagonjwa mahututi wa COVID-19 kutoka Ufaransa na amesema hilo ni uthibitisho kwamba mshikamano kati ya nchi wanachama unaendelea.


HII NI ORODHA YA NCHI ZILIZOATHIRIKA ZAIDI NA CORONA