- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: NCHI YA MAREKANI YAKUBWA NA TATIZO LA KUKATIKA KWA UMEME
Shughuli mbalimbali za biashara, usafiri pamoja na makazi jijini New York zilisimama kwa muda baada ya umeme kukatika jana jioni.
Taarifa zimesema karibu nyumba 70,000 pamoja na bishara zilikuwa gizani mjini New York . Huduma za usafiri wa treni za chini ya ardhi zilisimama na kuvuruga shughuli mbali mbali za burudani katika majira ya joto zilizokuwa zikiendelea mwishoni mwa wiki hii kwenye jiji hilo.
Gazeti la New York Times liliripoti kwamba jeshi la zima moto lilikuwa likipata simu kutoka maeneo mbalimbali ya watu waliokwama kwenye lifti. Kulingana na kikosi hicho, tatizo hilo limesababishwa na kuripuka kwa transfoma.
Mkuu wa kampuni ya kusambaza umeme mjini New York ya Con Edison, John McAvoy aliwaambia waandishi wa habari tatizo hasa lililosababisha transfoma hiyo kuripuka bado halijajulikana. Ni miaka 42 sasa tangu tatizo hilo lilipotokea tena Julai 13 mwaka 1977 siku ambayo kulikuwa na joto kali jijini New York hali iliyosababisha uporaji na ghasia.