Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 11:30 am

NEWS: NCHI YA BOTSWANA YARUHUSU MAPENZI YA JINSIA MOJA

Wakati kukiwa na Mvutano mkali katika taifa la Kenya baina ya Wanaharakati wa mapenzi ya jinsia moja na Serekali ya Uhuru Kenyatta Juu ya Uhalali wa wamapenzi ya jinsia moja nchini humo Nchi ya Botswana imekuwa ni taifa jingine la Afrika ambalo limebariki mapenzi ya jinsia moja baada ya mahakama kuu kutupilia mbali kipengele cha katiba ambacho kilikuwa kinakataza na kuadhibu hadi kifungo cha miaka 7 jela kwa watu watakaojihusisha na ushoga.

Image result for homosexual botswana

Punde baada ya uamuzi huo wa mahakama, wanaharakati wanaotetea mapenzi ya jinsia moja walisikika wakishangilia ndani ya ukumbi wa mahakama baada ya majaji wote waliokuwa wanasikiliza kesi hiyo kuridhia pasi na shaka kuondolewa kwa kipengele hicho cha sheria.

Uamuzi wa mahakama ya Botswana umekuja wakati huu karibu nusu ya mataifa yaliyoko kusini mwa jangwa la Sahara yanasheria kali zinazokataza mapenzi ya jinsia moja.

Mapema mwaka huu nchi ya Angola na yenyewe iliruhusu mapenzi ya jinsia moja ikifuta sheria ya awali iliyokuwa ikilitaja kuwa kosa la jinai kwa mtu au watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja maarufu kama Ushoga.

Image result for hormosexial Botswana

Waliowasilisha kesi mahakamani walidai kuwa sheria zilizokuwepo zilitungwa wakati wa ukoloni na kwamba watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja wamekuwa wakitengwa na wakati mwingine maisha yao kuwa hatarini.