Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 7:30 pm

NEWS: NCHEMBA: SERIKALI YAJIPANGA KUTHIBITI AJALI ZA BODABODA

DODOMA: BUNGE limeelezwa kuwa katika kipindi cha miaka mitatu, jumla ya ajali 5,418 za bodaboda zilitokea na kusababisha vifo vya watu 1,945.

Takwimu hizo za ajali ni kuanzia Januari 2015 hadi Februari 2017.

Hayo yalibainishwa jana Bungeni na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kaliua(CUF), Magdalena Sakaya.

Sakaya alitaka Kujua ni ajali ngapi za bodaboda zimetokea kwa miaka mitatu tangu mwaka 2015 mpaka 2017 na ni watu wangapi wamepoteza maisha kwenye ajali hizo na walemavu ni wangapi.

“Je, serikali ina mikakati ya uhakika ya kuokoa maisha na nguvukazi ya Taifa inayopotea kwa usafiri huo, ”amehoji Sakaya

Akijibu swali hilo, Nchemba amesema mbali na vifo pia ajali hizo zimesababisha majeruhi na walemavu 4,696.

Amesema serikali kupitia jeshi la polisi inayomikakati ya kuokoa maisha na nguvu kazi ya Taifa inayopotea kutokana na ajali za bodaboda.

Ametaja mikakati hiyo kuwa ni pamoja na kupitishwa kwa kanuni ya leseni za pikipiki za kubeba abiria mwaka 2009, kutoa elimu ya usalama barabarani mashuleni na kupitia vipindi vya radio, televisheni na vipeperushi.

Aidha alisema mikakati mingine ni kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwa waendesha bodaboda, kuimarisha usimamizi wa sheria za barabarani, kusisitiza madereva wa bodaboda kuepuka kuendesha kwa mwendo kasi.

“Pia kuepukanvitendo vya ulevi, kuweka viakisi mwaka ili kuonekana kwa urahisi na kusisitiza matumizi ya kofia ngumu ili kupunguza madhara yanayosababishwa na ajali,”Amesema