Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 11:33 pm

NEWS: NASSARI AAHIDI KUPELEKA SPIKA MAHAKAMANI KUDAI HAKI YAKE

Dar es salaam: Aliyekuwa Mbunge wa Arumeru mashariki Joshua Nassari amesema amepanga kwenda kufungua jalada mahakamani kudai haki yake ya kuvuliwa ubunge dhidi ya Spika wa Bunge Job Ndugai.

Nassari alivuliwa Ubunge na Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Job Ndugai kwa madai kuwa mbunge huyo amepoteza sifa za kuwa mbunge baada ya kutohudhuria vikao vitatu vya bunge mfululizo.

Akiongea leo Jumapili Machi 17, 2019 na waandishi wa Habari Nassari amesema kuwa Tarehe 27 siku ambayo mke wake alijifungua mtoto siku ya pili 28 ndio ilikuwa siku ya kuanza kwa mikutano ya Bunge kwahiyo alitakiwa kuchagua aidha kwenda bungeni kwa ajili ya kuhudhuria vikao au kubaki na kumuuguza mkewe ambaye anadai alikuwa mahututi "nilikuwa na machaguo mawili tu nimwache mke wangu akiwa mahututi niende nikasaini posho bunge au kumuuguza mke wangu." amesema Nassari “Ieleweke kwamba ukiwa Mbunge haiondoi Ubinadamu wa kawaida wala haiondoi majukumu mengine ya kifamilia kama Binadamu mwingine yeyote” ameongeza Nassari

Spika nduagai alimfuta ubunge Mbunge huyo tarehe 14 machi 2019 na kumuandikia barua Mwenyekiti wa NEC Jaji Semistocles Kaijage kumtaarifu kuwa jimbo la Arumeru Mashariki linaloongozwa na mbunge huyo liko Wazi kwa sasa hivyo aandae mazingira ya Mchakato wa Uchaguzi

Spika alisema kuwa alichukuwa uwamuzi wa kumfuta ubunge Mbunge huyo Kijana kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 71(1) (c) ibara hiyo inaeleza kuwa mbunge atakoma kuwa mbunge na ataacha kiti chake kama mbunge ikiwa ataacha kuhudhuria mikutani mitatu ya Bungu mfululizo bila kibali cha Spika.