Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 2:59 pm

NEWS: NAPE AWATAKA WALIOHUJUMU KOROSHO KUCHUKULIWA HATUA KABLA YA KUWATAJA

Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye (CCM) ameitaka Serekali kuwashughulikia wale wote waliohusika na kuhujumu Korosho kwa kufanya mambo ya hovyo wachukuliwe hatua kali na wasipochukuliwa ataleta kusudio kuonesha jinsi walivyofanya mmoja mmoja.

Image result for nape bungeni

Kauli hiyo ya Nape ameitoa leo,Mei 20 bungeni,wakati akichangia mjadala wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo, kwa mwaka wa fedha 2018-2019.

“Watu waliofanya hovyo wanajulikana na kama wasipochukua hatua wenyewe, wasipofanya tutaleta kusudio jinsi walivyofanya mmoja mmoja na jinsi ambavyo wanatakiwa kuchukua hatua kwa sababu waliyoyafanya ni kuhujumu,Korosho,wananchi lakini pia ni kuhujumu uchumi wa Nchi.

Nape amesema Rais alikuwa na nia njema lakini walioenda kuitekeleza wameenda kuiua sekta ya Korosho.

“Hivi tunavyoongea Mheshimiwa Spika bahati mbaya zoezi lilikuwa na dhulma,lilikuwa na rushwa lilikumbwa na ubabaishaji mwingi na uongo mwingi sana.

“Hivi tunavyoongea Jimbo la Mtama peke yake kwenye vyama vya msingi 11 wakulima ambao wana korosho chini ya tani 1500 ambao wamehakikiwa mashamba yao zaidi ya 1281 kwa miezi nane tangu Korosho yao ichukuliwe hawajapa hata senti tano.

“Lakini Korosho yao imechukuliwa hawana fedha za kutengeneza mashamba yao, Nape alisema mapendekezo yake ni iletwe sheria ya Korosho yote ili ipitiwe upya. “Kile kipengele tulichokinyofoa kimetuletea shida sana sasa leteni sheria yote tuipitie.

“Napendekeza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali aende kukagua atuletee ripoti hapa ndani namna zoezi lilovyoenda ili tuchukue hatua ya kuziba mapengo.

“Kama nilivyosema Rais wengi wamemdanganya sasa ni vizuri wawajibike na Mheshimiwa Spika ni vizuri tukawa ‘Specific’ si sahihi kuiingiza Serikali katika mambo yaliyofanyika hovyo.

“Leo tukiulizana Korosho yetu ipo wapi haiwezi kukaa zaidi ya miezi sita hapa nchini ikabaki salama mngetuambia kuna korosho sahihi, huu ni uongo na tukiendelea kuusema huu uongo na bado tunaendelea kubaki hatutabaki salama,amesema Nape.