- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: NAMNA MEMBE ALIVYOWASILI KUHOJIWA
Dar es Salaam. Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Njee nchi Tanzani, Bernard Membe amewasili katika ofisi za makao makuu ya CCM mjini Dodoma leo Asubuhi Saa 3 Februari 6, 2020 kwa ajili ya kuhojiwa kuhusu tuhuma za kimaadili zinazomkabili.
Membe amewasili katika ofisi hizo maarufu ‘white house’ akiwa katika gari aina ya Range Rover jeusi(Vouge)
Membe aliyevaa suruali nyeusi na shati lenye michirizi mieusi na kijani, alipokelewa na watu mbalimbali na Kusaliamiana na wengine aliowakuta nje, kisha kuingia ndani ya jengo hilo lililopo Jiji la Dodoma.
Jana waziri huyo wa zamani wa mambo ya nje alieleza kuwa kikao hicho kitakuwa muhimu kwake akitumia neno, “nilikuwa nakisubiri sana.”
Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM iliyoketi Desemba 13, 2019 iliagiza makada watatu wa chama hicho waitwe na kuhojiwa na Kamati ya Maadili na Usalama ya chama hicho baada ya kutuhumiwa kwa makosa ya kwenda kinyume na taratibu za chama.
Akizungumza katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Azam jana, Membe amesema ana amini kikao hicho kitakuwa kigumu huku akitumia neno ‘itategemea’, akimaanisha uamuzi utakaotolewa na kamati hiyo baada ya kumhoji.
Juzi, ikiwa ni siku 52 zimepita tangu CCM kutangaza kuwaita wanachama wake watatu kuhojiwa, Membe aliandika katika ukurasa wake wa Twitter, “hatimaye, nimepokea barua ya kuitwa kwenye kikao cha kamati ndogo ya udhibiti na nidhamu jijini Dodoma.”
Katika akaunti ya Twitter, ambayo mara kadhaa imekuwa ikitoa taarifa kuhusu mwanadiplomasia huyo, kuliandikwa: “Kikao kitafanyika Februari 6, 2020 saa 3 asubuhi kwenye jengo la White House. Nitahudhuria bila kukosa na bila kuchelewa! Stay tuned!”
Wengine ambao wanapaswa kuhojiwa na kamati ya maadili ya CCM ni makatibu wakuu wa zamani wa chama hicho tawala nchini Tanzania, Abdulrahman Kinana na Yussuf Makamba
Alipoulizwa na mtangazaji aliyekuwa akimhoji kama atakuwa tayari kwa uamuzi wowote, Membe alijibu kwa ufupi, “Itategemea.”
Kuhusu jopo litakalomfanyia mahojiano, amesema kikao hicho kitaongozwa na makamu mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula, akidai mahojiano kuwa mazuri, yenye uwazi huku akitamani ushiriki wa wanahabari katika mahojiano hayo.
“Ninawaambia watanzania, kesho ni siku muhimu sana, nilikuwa ninaisubiri sana kukutana na hii kamati na ninamuomba Mungu anijaalie niwepo katika kamati kwa sababu nitapata nafasi ya kuzungumza na wanakamati mambo wasiyoyajua na wanayoyajua.”
“Kwa hiyo kesho (leo) saa tatu asubuhi nisikosekane kwenda , niko sasa safarini kwenda Dodoma ili kesho (leo) tukazungumze. Kamati itasikiliza hoja na watatoa mapendekezo kwa halmashauri kuu ya Taifa ambayo itaamua kutoa uamuzi wowote, nadhani uamuzi utatoka mwishoni mwa mwezi huu Februari au Machi,” amesema Membe.