- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: NAMNA CAG ALIVYOWASILI BUNGENI KUHOJIWA NA KAMATI
Dodoma: Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad leo asubuhi Januari 21, 2019 amefika mbele ya kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge kwa ajili ya kuhojiwa kuhusu kauli yake ya “udhaifu wa Bunge.”
CAG Assad ameitwa mbele ya kamati hiyo kujieleza kuhusu kauli aliyoitoa wakati alipokuwa akihojiwa na kituo cha televisheni cha idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa (UN) akiwa New York, Marekani alikokuwa akihudhuria mkutano.
Alitumia neno “udhaifu” wa Bunge alipokuwa akieleza sababu za kutofanyiwa kazi kwa ripoti zake ambazo zimekuwa zikibainisha ufisadi.
Mara baada ya kuingia katika ukumbi yanapofanyika mahojiano hayo saa 5:01 asubuhi, CAG aliyekuwa amebeba begi dogo jeusi, aliwasha kompyuta yake mpakato na kisha kuwasalimu wajumbe wa kamati hiyo.
Alifika katika viwanja vya Bunge saa 4:49 asubuhi akiwa peke yake bila wasaidizi, akateremka katika gari jeupe na kupita katika mashine za ukaguzi.
Katika mashine hizo Profesa Assad alivua viatu, koti, saa, miwani na kisha kuvaa tena vitu hivyo baada ya ukaguzi.
Huku ulinzi ukiwa umeimarishwa, baada ya ukaguzi Profesa Assad alikwenda kuketi eneo la mapumziko na msaidizi wa Spika, Said Yakubu alimpelekea kitabu cha kusaini