- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: NAIBU WAZIRI MASAUNI AAGIZA KUSIMAMISHWA KAZI ASKARI 4
Mbeya: Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amemuagiza Kamishna wa Jeshi la Magereza kuwasimamisha kazi askari wanne wanaodaiwa kushirikiana na wafungwa kuingiza dawa za kulevya aina ya bangi pamoja na simu za mkononi Ndani ya Gereza hilo
Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Machi 22, 2019 mkoani hapa Masauni amesema amebaini jambo hilo baada ya kufanya ziara ya siku moja katika gereza hilo. “Jana nilitembelea Gereza la Ruanda na kugundua askari kukosa maadili kwa kuwa wamekuwa wakishirikiana na wafungwa kuingiza bidhaa haramu. Naagiza askari hawa wasimamishwe kazi ili kupisha uchunguzi wa kina,” amesema Masauni.
Waziri amemtaka kamishna huyo kuunda kamati ya kuchunguza mtandao wa kuingiza bidhaa hizo. “Nilikamata simu 10 na na dawa za kulevya aina ya bangi.
Huu ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu Rais (John Magufuli) ametoka kukemea vitendo hivyo lakini bado wanaendelea,” amesema Masauni. “Vitu nilivyovibaini vyote niliwakabidhi polisi kufanya uchunguzi na bahati nzuri ripoti ya uchunguzi nimekabidhiwa muda huu.”