Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 12:52 pm

NEWS: NAIBU WAZIRI BASHE ATOA MAAGIZO KWA VYAMA VYA USHIRIKA NCHINI.

DODOMA: Naibu waziri wa kilimo Hussein Bashe ameagiza viongozi wote wa vyama vya ushirika ambao sio wakulima kuondolewa kwenye nafasi zao, na kutaka viongozi wa vyama hivyo lazima wawe miongoni mwa wakulima.

Pia ameeleza kuwa Wizara inamipango ya kuimarisha vyama vya ushirika hapa nchini na kuhakikisha wakulima wananufaika na jasho lao.

Bashe ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na wakulima katika mkutano wa kitaifa wa wakulima wadogo Tanzania ambapo amesema ili kuleta matokeo chanya lazima wapatikane viongozi husika wenye weledi katika maswala yote yanayohusu kilimo.

Aidha ameongeza kuwa wizara ya kilimo iko kwenye mchakato wa mradi mkubwa wakwenda kidigitali kwa kutoa huduma ya kupiga simu bure pamoja na ujumbe mfupi wa maandishi kwa wakulima ili kuwasiliana moja kwa moja na wizara ili kupunguza upungufu wa maafisa ugani vijijini.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Wakulima Wadogo Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma JUWACHA linalofadhiliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la ActionAid Janeth Nyamayahasi ametoa ushauri kwa serikali kusimamia sheria inayozitaka serikali za mitaa kutenga asilimia 20 kwenye kilimo na asilimia 15 kwenye mifugo ya mapato ya ndani kwa ajili ya shughuli ya maendeleo ya ndani.

Mkutano huo wa siku mbili umewakutanisha wakulima wadogo kutoka maeneo mbalimbali nchini kujadili changamoto katika sekta ya kilimo huku ukibeba kauli mbiu inayosema “Fungua Fursa kwa ukuaji wa sekta ya kilimo na maendeleo kupitia bajeti jumuishi.”