- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: NAIBU WAZIRI AWESO AWATAKA WATENDAJI WA RUWASA KUFANYAKAZI KWA BIDII.
GEITA: Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amesisitiza uwajibikaji kwa watendaji wa Wakala ya Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) na kusema Wizara ya Maji imewasimamisha Wahandisi wa Maji 67 kwa kushindwa kutimiza majukumu yao kwa weledi na kusababisha ujenzi wa miradi ya maji kukwama.
Lengo la kuwasimamisha kazi wahandisi hao ni kuongeza uwajibikaji kwa wataalam wanaosimamia ujenzi wa miradi ya maji katika maeneo mbalimbali, iweze kuleta tija
kwa kufikisha huduma ya maji kwa wananchi.
Mhe. Aweso ametoa ufafanuzi huo wakati akiwa ziarani katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita, mkoani Geita mara baada ya kukagua ujenzi wa Mradi wa Maji wa
Chankorongo uliogharimu kiasi cha Shilingi bilioni 4.9 na kuhudumia vijiji vya Chankorongo, Chigunga, Nyakafulo, Kabugozo na Chikobe vilivyopo katika Kata ya Busanda.
‘‘Naamini Wakala ya Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) itakuwa suluhisho la tatizo la utekelezaji wa miradi ya maji vijijini kwa sababu tumewasimamisha
kazi wahandisi 67 na kubaki na wahandisi wazuri na wenye uwezo wa kutekeleza majukumu yao kwa weledi’’, Aweso amesema.
‘‘Kupitia RUWASA tutaleta mapinduzi makubwa vijijini kuanzia hatua ya usanifu, ujenzi na usimamizi wa miradi kutokana na mabadiliko makubwa ya mfumo, ambapo awaliulikuwa kikwazo kwa miradi ya maji vijijini kufanikiwa’’, Aweso amesema.
Vilevile, Mhe. Aweso amekagua miradi ya maji ya Manga, Kasamwa na Bulela katika Mji wa Geita akiwataka wahandasi wa maji kutimiza wajibu wao na kufanikisha azma ya
Mhe. Rais Magufuli ya Kumtua Mama Ndoo Kichwani.
Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Aweso ametoa rai yake kwa wananchi kuchangia huduma ya ya maji ili miradi iweze kujiendesha kwa mafanikio na kudumu kwa muda
mrefu, ikiwemo kuwa waaminifu na fedha zinazotokana na makusanyo yanayotokana na mauzo ya maji.
Akisisitiza fedha hizo ni lazima ziwe na utaratibu mzuri wa mapato na matumizi kwa kamati za maji, kinyume na hapo miradi iliyogharimu Serikali fedha nyingi za ujenzihaitakuwa msaada kwa wananchi.