Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 7:38 am

NEWS: NAIBU WAZIRI AWESO AMTUPA NDANI MHANDISI MONDULI

NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji , Jumaa Aweso ameamuru kukamatwa na kuwekwa mahabusu kwa Mhandisi wa Maji wa wilaya ya Monduli ,Charles Saidea na Mkandarasi kutoka kampuni ya Meru Constructions ,Ayo Jeremia kwa tuhuma za kufanya udanganyifu katika miradi wa maji inayoendelea katika vijiji 10 vya Halmashauri ya wilaya ya Monduli .

Askari Polisi akiwa amewashikilia ,Mhandisi wa Maji wa wilaya ya Monduli,Charles Saidea (kulia) na Mkandarasi ,Ayo Jeremia wa kampuni ya Meru Constructions mara baada ya Naibu Waziri Jumaa Aweso kuamuru wakamatwe kutokana na kubainika kufanya udanganyifu katika mradi huo

Aweso ametoa agizo hilo katika kijiji cha Lendinyika wakati wa ziara yake ya siku moja katika wilaya ya Monduli kukagua utekelezaji wa Miradi ya Maji katika vijiji 10 vya Halmashauri hiyo,ziara ambayo hata hivyo alilazimika kuikatisha mara baada ya kubaini kuwepo kwa taarifa zinazo kinzana na taarifa ya utekelezaji wa mradi wa maji wenye thamani ya Sh Bil 1 na Mil 79