Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 6:43 pm

NEWS: NACTE YAVIFUTIA USAJILI VYUO 10 NCHINI TANZANIA

Dar es salaam. Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi nchini Tanzania (Nacte) limevifutia usajili vyuo 10 vya ufundi nchini humo kwa sababu ya mapungufu mbalimbali yalioonekana licha ya kuonywa miaka miwili iliyopita bila kufanya maboresho.

Uwamuzi huu umetangazwa leo Februari 10, 2020 na mkurugenzi wa uthibiti, ufuatiliaji na tathmini wa baraza hilo, Dk Jofrey Oleke. Dk Oleke mara baada ya NACTE kufanya ukaguzi wa vyuo 105 kati ya Oktoba na Desemba, 2019. Mchanganuo wa vyuo hivi unahusisha vyuo saba vilivyofutiwa usajili

Kati ya vyuo hivyo kipo cha uandishi wa habari cha Times(TSJ) ambacho hakijafanya udahili wa wanafunzi tangu mwaka 2017/18. Vingine ni Chuo cha mafunzo ya ufundi ERA(Bukoba), Chuo cha mafunzo ya usimamizi Azania(Dar es Salaam) , Chuo cha Clever( Dar es Salaam), Chuo cha mafunzo cha ACES (Zanzibar), taasisi ya mafunzo ya biashara, utafiti na teknolojia ZIBRET (Zanzibar) na taasisi ya mafunzo ya masuala ya kijinsia(Dar es Salaam).

Dk Oleke amesema upungufu uliobainika wakati wa ukaguzi ni uhaba na ubora hafifu wa walimu, uhaba wa vitendea kazi vya kujifunzia na kufundishia pamoja na miundombinu isoyokidhi vigezo

Vyuo viwili vimefutiwa usajili baada ya kukosa uwezo wa kujiendesha ni chuo cha mafunzo ya biashara na usimamizi (Dar es salaam) na kituo cha mafunzo ya Kompyuta (UCC) Mwanza. Chuo cha Kilimo Kizimbani kinakamilisha idadi ya vyuo vilivyofutiwa usajili baada ya kuwa sehemu ya Chuo Kikuu cha Zanzibar (Suza). "Tunafuta usajili wa vyuo hivi kuanzia leo, lakini vinaweza kurekebisha kasoro na kuomba tena kusajiliwa upya lakini Itabidi kujiridhisha ndiyo tutoe usajili upya," amesema Dk Oleke.

Nacte hufanya ukaguzi kila baada ya miezi mitatu kwa awamu katika Kanda zake nane kote nchini. Kwa mujibu wa Nacte, idadi ya vyuo vilivyopo chini ya baraza kabla ya kufuta usajili wa vyuo hivyo ilikuwa ni 439.