- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MWIZI AWAIBIA MATRAFIKI PESA WALIZOKUSANYA ZA RUSHWA
Mwanaume mmoja mwenye ujasiri Mkubwa nchini Kenya amewaibia polisi wa Barabarani kitita cha Pesa kisichojulikana walizokuwa wamekusanya kama rushwa kutoka kwa madreva wa magari nchini Humo.
Kwa mujibu wa habari zilizochapishwa kwenye mtandao wa gazeti la Nation, mwizi huyo alizuka gahfla kutoka msituni, akanyakua kifurushi kilichokuwa na pesa kando mwa barabara na kisha kuchana mbuga kwa kasi.
Kisa hicho kisicho cha kawaida kilitokea siku ya Jumatano majira ya saa saba kwenye barabara kuu ya Embu kuelekea Nairobi, katika mkoa wa kati mwa Kenya.
Mwendesha gari mmoja aliyeshuhudia kisa hicho alisema polisi wa trafiki mwanaume alijaribu kumfuata mwizi huyo bila mafanikio.
Kwa mujibu wa dreva huyo, mwizi huyo alikuwa anakimbia kwa kasi ambayo ilimwacha polisi akihema baada ya kujaribu kumfuata ili aokoe hela.
Polisi huyo na mwenzake wa kike walibaki vinywa wazi huku donge lao la siku likitoweka wakitazama tu!
Wengi mitandaoni wanawakejeli polisi kwa kuwapendekeza kwamba yafaa wabuni mbinu mpya ya kuhifadhi pesa wanazopokea kama rushwa wakiwa kazini