- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MWINYI AKASIRISHWA, MAKAMBA KUTUMIA PICHA YAKE BAADA YA KUTUMBULIWA
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi ameelezea kutofurahishwa kwake na kitendo kilichofanywa na aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba kutumia picha yake aliyepiga na Mbunge huyo katika mitandao ya kijamii muda mfupi baada uteuzi wake kutenguliwa na Rais Magufuli .
Mzee Mwinyi amesema picha iliyotumiwa na January Makamba katika mitandao ya kijamii ikimuonesha yeye ameketi na January Makamba wakicheka muda mfupi baada ya kufukuzwa Uwaziri imemkwaza kutokana kutumiwa katika mazingira na wakati usiostahili ."kwakeli sikuipenda, sikuipenda kuona kitu kama kile katika mazingira haya, picha za namna ile ni kawaida, watu wengi wanakuja kuniona hapa tunazungumza wanasema tupate picha. ''lakini kupiga picha katika hali hii halafu mnaonekana mnanong'onezana, mnanong'onezana nini?" alisema Mzee Mwinyi
Mzee Mwinyi anasema picha hiyo ilipigwa zamani wakati January Makamba alimpomtembelea kwa ajili ya kupata uzoefu wake kwa kuwa nae aliwahi kuwa Waziri wa Muungano na Mazingira na pia alikwenda kumuomba aandike dibaji katika kitabu chake
January Makamba, aliyehudumu katika nafasi ya waziri wa Mazingira na Muungano nchini Tanzania alivuliwa wadhifa huo hapo jana.
Taarifa ya Ikulu Tanzania haijaeleza sababu ya Makamba kutenguliwa na nafasi yake sasa kuchukuliwa na George Simbachawene.
Punde baada ya kutangazwa kutenguliwa kwake, Makamba aliweka picha yake akiwa amekaa na Mzee Mwinyi katika mtandao wa Twitter iliyoambatana na ujumbe:
"Ni kweli nimeyapokea mabadiliko yaliyofanywa kwa moyo mweupe kabisa kabisa. Nitasema zaidi siku zijazo." Huku akiambatanisha maneno hayo na picha yake na rais msaafu Ally Hassan Mwinyi wakiwa wanaangua kicheko.