Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 4:28 am

NEWS: MWIGULU NCHEMBA WAZIRI MPYA WA KATIBA NA SHERIA

Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli amemteua Mbunge wa Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, uteuzi huo unaanzia leo Mei 02, 2020.

Mwigulu Nchemba anachukua nafasi ya marehemu Balozi Dkt.Augustine Mahiga aliyefariki jana 01 Mei, 2020 na Kuzikwa hii leo nyumbani kwao Tosamaganga Mkoani Iringa.

Mwigulu aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya ndani na alitenguliwa uteuzi wake na Rais Magufuli Mnamo Julai 1, 2018.