Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 12:40 pm

NEWS: MWIGULU AAHIDI KUTATUA CHANGAMOTO YA MAGARI YA ZIMAMOTO

DODOMA: WAZIRI wa mambo ya ndani ya nchi MWIGULU NCHEMBA ameahidi kukaa na wizara ya Fedha na Mpango ili kukubaliana namna bora ya kuhakikisha changamoto ya ukosefu wa magari ya zimamoto nchini inatatuliwa kwa haraka.

MWIGULU amesema hayo leo mjini Dodoma wakati akifungua kikao cha mwaka cha maafisa wakuu wa Jeshi la Zimamoto Tanzania Bara.

MWIGULU amesema serikali inafahamu changamoto hiyo na inaendelea na taratibu mbalimbali ili kuweza kuzitatua.