Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 3:56 am

News: Mwenyekiti wa mtaa amshukia mkuu wa wilaya kwa madai yakushindwa kutafuta ufumbuzi wa millioni 14 zilizotafunwa.

Dodoma: Ismail Seifu (CUF) ambaye ni mwenyekiti wa mtaa wa Mlimwa Kusini amemshukia Mkuu wa wilaya ya Dodoma,Christina Mdeme kwa kushindwa kutafuta ufumbuzi wa milioni 14 zilizotafunwa na wajanja wachache lakini anakomaa na milioni Moja isiyo na ushahidi.

Seifu ambaye alitangazwa kusimamishwa nafasi hiyo na kukabidhi ofisi ya mtaa ndani ya siku saba kwa amri ya Mkuu wa wilaya,amesema kuwa hawezi kukabidhi ofisi kutokana na Mkuu wa wilaya kutotimiza vigezo vya kumsimamisha.

Akizungumza na vyombo vya habari Seifu amesema anamshangaa Mkuu wa wilaya ya Dodoma kushindwa kutafuta ufumbuzi wa baadhi ya viongozi ambao walifanya ufisadi wa sh.milioni 4 za mradi wa kunusuru kaya masikini TASAF,ubadhilifu wa milioni kumi za ujenzi na upimaji wa viwanja huku ushahidi ukiwa wazi lakini akija na hoja dhaifu za kutaka kumsimamisha mwenyekiti kwa tuhuma za ubadhilifu wa milioni moja isiyo na ushahidi.

"Nataka kuwaelezea waandishi wa habari kuwa licha ya rais kuwa na nia njema lakini wapo watu wanaomwangusha,nimeanza muda mrefu kumwandikia mkuu wa wilaya barua ya kulalamika juu ya wizi wa pesa za mradi wa Tasaf lakini amenyamaza kimya.

"Nikamwandikia barua ya kuomba ukaguzi wa kufanya ukaguzi wa mtaa wa Mlimwa Kusini kuna ubadhirifu wa milioni kumi amekaa kimya.

"Sasa nashangaa kuona amekurupuka na hoja dhaifu alizopelekewa na wajumbe wangu ambao kwa ubadhilifu wao ndani ya kamani niliwateua na kuwatengua na kuwapeleka mahakamani na wakakutwa na hatia ya kufungo cha mwezi mmoja na faini ya 50,000 kila mmoja wakisingizia kuwa mimi nimekula milioni moja ambayo haina ushahidi"alieleza Seifu.

Barua yenye kumb.Na AB.380/507/01/17 ya tarehe 6 Februari ikiwa na kichwa cha Habari kilichoandikwa "Taarifa ya ukaguzi ulifanyika Mlimwa Kusini-Kata ya Ipagala"ilimtaka mkurugenzi kutoa malalamiko hayo haraka iwezekanavyo,na barua hiyo ilisahiniwa na Katibu tawala wilaya Dodoma Jasinta V Mboneko.

Amesema tuhuma zinazomkabili ni ujenzi wa ofisi ya mtaa bila kufuata taratibu za kutangaza tenda,kuuza vibanda kimoja zaidi ya mtu mmoja jambo ambalo linaweza kusababisha uvunjifu wa amani,na matumizi mabaya ya sh.milioni moja.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Dodoma,Christina Mdeme,amesema yeye anayo mamlaka ya kumsimamisha.

Kuhusu ukaguzi wa milioni kumi za mtaa amesema ni muhimu kufanyika kwani pesa za serikali kupotea bure.