Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 8:32 pm

NEWS: MWENYEKITI WA CLUB YA SIMBA SWEDI MKWABI AJIUZULU WADHIFA WAKE

Mwenyekiti wa Klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba Sport Club Swedi Mkwabi amejiuzulu wadhifa wake kama mwenyekiti wa club hiyo,

Kwamujibu wa taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari leo Septemba 14, 2019 na club hiyo inasema kuwa Mkwabi aliiandikia barua bodi ya wakurugenzi kuptia kwa mwenyekiti wa bodi hiyo Mohammed Dewji ya kuomba kujiuzulu wadhifa huo.

Tokeo la picha la swedi mkwabi na wandishi

"sababu kuu ya kijiuzulu nafasi hiyo ni kuhitaji muda zaidi kusimamia shughuli zake binafsi." ilisema sehemu ya Taarifa hiyo

"Bodi ya Wakurugenzi na Sekretarieti ya Simba inamtakia kila la heri katika shughuli zake, na tunatumaini kwamba ataendelea kushiriki katika shughuli mbalimbali za klabu kama ilivyokuwa awali. Utaratibu wa kumpata Mwenyekiti mpya tutawatangazia hapo baadae." imesema taarifa hiyo ya Simba.

SABABU ZA KUJIUZULU KWA MKWABI

Mkwabi na mwekezaji Mo Dewji kwa muda sasa wamekuwa hawaelewani kiasi ambacho kinapelekea sintofahamu ndani ya Simba.

Inaelezwa kuwa Mo Dewji alikuwa hana Imani na Mkwabi kutokana kuonekana kuwapa nguvu kundi linalompinga likiongozwa na Mzee Kilomoni , Mo anaamini Mkwabi anavujisha Siri za vikao ndani ya Simba kwa kina Mzee Kilomoni kiasi kwamba imekuwa ngumu kupata hati inayoshikilia mzee Kilomoni

Hali ya ugomvi wa Mkwabi na MO ulionekana wazi mara baada ya MO kuanza kuandika mfululizo wa ujumbe mbalimbali zenye "mafumbo" katika kurasa zake za kijamii na kuzidisha mijadala miongozi mwa wanachama, mashabiki wa Simba na wadau mbalimbali wa soka hapa nchini.

"Kwenye uongozi, na kwenye maisha, huwa nakaribisha kukosolewa. Lakini siwezi na sikubali kufanya kazi na mtu anayejuhumu malengo, mipango na maslahi mapana ya taasisi, mtu anayetoboa mtumbwi tunaosafiri nao," MO aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake huku akiweka picha inayomwonyesha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (kushoto) na kulia ni Mwenyekiti wa Simba, Swedi Mkwabi.

Siku chache zilizopita ugomvi ulipamba Moto zaidi baada ya Simba kuingia mkataba na moja ya makampuni ya Mo inayosimamia Dada yake Fetima Dewji kupitia kinywaji Cha Mo Extra. Mwaka Jana Simba iliingia mkataba na kampuni hiyo ya A one kupitia kinywaji Cha Mo Energy wenyw thamani ya milioni 250 na pesa yote ilitangwaza itapelekwa kwenye ujenzi wa uwanja Bunju na mwaka huu mwezi wa pili Simba ilipaswa kuanza mazoezi kwenye uwanja huo kitu ambacho hazijakamilika mpaka sasa.


Mkwabi alilalamika kwa wazee wa Simba kwamba timu imeingia mkataba mpya hata yeye Mwenyekiti upande wa wanachama hajui Wala hajashirikishwa wakati mkataba wa awali pesa haijulikani ilivyotolewa na kutumika (Kama screenshot inavyojieleza). Mkwabi amekuwa akililalamika kumekuwa na mgongano wa maslahi kwenye kubageini Kati ya Mo Dewji Mwenyekiti wa bodi na Mo Dewji mdhamini kupitia kampuni yake ya A one, imekuwa rahisi kwa Mo kupitisha kampuni yake kwenye udhamini kwa pesa kidogo maana yeye pia ndo Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Simba.


Mo anaamini Mkwabi anatumia nafasi yake kuwapa nguvu wanaompinga maana wamekuwa wanajua Kila hatua wanaopiga
Mpaka Sasa Mo amesema ameshatumia bilioni 5 na amesema akijitoa hata dai pesa hizo atasemehe tu na kuendelea na Mambo yake mengine.

"Kulingana na Ugomvi huo Mkwabi ameona kukaa pembeni ili kuepusha gharama kubwa zinazoweza kutokea kwenye club hiyo" alisema mmoja wa wajumbe wa Bodi ya Simba alipozungumza na Muakilishi MEDIA kwa sharti la kutotajwa jina lake.