Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 7:33 pm

NEWS: MWENYEKITI WA CCWT ASWEKWA RUMANDE KWA AMRI YA DC

MBEYA : MWENYEKITI wa Chama cha Wafugaji (CCWT) wilaya ya Chunya mkoani Mbeya,Shang’a Laboy amewekwa ndani kwa saa 28 kwa amri ya mkuu wa Wilaya hiyo Rehema Madusa kuwa mwenyekiti kuwashawishi wafugaji kutolipa kiasi cha sh.1000 kwa ajili ya kupiga chapa mifugo yao.

Mkuu wa wilaya hiyo amesema amelazimika kumweka ndani mwenyekiti huyo kutokana na kuwagomesha wafugaji kutoa shilingi 1000 kwa ajili ya kupiga chapa mifugo yao huku akifafanua kuwa bei elekezi ya serikali ya kupiga chapa ni sh.500 ila mkoa ulikubaliana kulipa kiasi cha sh. 1000.

Madusa ameeleza kuwa bei ya mkoa ya kuchangia upigaji wa chapa ni kiasi cha sh.1000 na kuongeza kuwa mfugaji yoyote ambaye atashindwa kuchangia mifugo yake kwa bei y ash.1000 hatatambuliwa kama mkazi wa Chunya .

“Ninajua kuwa bei elekezi ya Serikali ya kuchangia kupiga chapa mifugo ni sh.500 lakini Mkoa tuliweka utaratibu wa kuchangia sh.1000 kila mfugo, na hiki ni kiwango kidogo kwa wilaya ya chunya kwani wapo wengin ambao wanachangia hat ash.3000.

“Pia mapendekezo hayo ya kuchangia sh.1000 yalipitia katika vikao vya baraza la halmashauri na kupewa Baraka zote ili wafugaji waweze kuchangia kiasi hicho.

“Hali hiyo ilitokana na kuwepo kwa migogoro ya mara kwa mara kati ya wafugaji na wakulima lakini pia wafugaji kwa wafugaji kutokana na wakati wingine kugombania mifugo kutokana na mifugo yao kutokuwa na halama yoyote na kusabisha migogoro”amesema Madusa.

Katika hatua nyingine Madusa amesema pesa ambazo zimekuwa zikikusanywa kutokana na pesa hiyo ambayo ni ya kupiga chapa mifugo zinatumika kwa kuwalipa watu ambao wapo katika maeneo ya kazi ikiwa ni pamoja na kuwapatia posho wale wote ambao wamekuwa wakitoa elimu kwa wafugaji.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama cha wafugaji wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya,Shang’ai Laboyi amesema kuwa yeye amelazimika kuwaambia wfugaji kutokutoa kuwango cha sh.1000 badala yake watoe sh.500 ambao ndiyo bei elekezi ya serikali kwa kupiga chapa ya mifugo.

“Imekuwa siyo jambo jema kuwatoza fedha kiasi cha sh.1000 wakati bei elekezi ya serikali ni sh.500 na ikumbukwe kuwa inawezekana mtu akawa na mifugo mingi hivyo akiwa na mifugo mingi atalazimika kuta fedha nyingi jambo ambalo litaonekana kuwa gumu zaidi kulingana na uchumi wa sasa” amesema Laboy.