- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MWENYEKITI WA CCM (UWT) ABURUZWA MAHAKAMANI KWA KUFOJI CHETI
Dar es salaam; Aliyewahi kuwa mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa chama cha mapinduzi CCM (UWT) Wilaya ya Ilala, Norah Waziri maarufu kama Nora Mzeru leo Ijumaa Julai 12, 2019 amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni akikabiliwa na shtaka la kughushi cheti chake cha ndoa.
Kwa mujibu wa Wakili wa Serikali, Benson Mwaitenda amedai mbele ya Hakimu Mkazi, Anifa Mwingira kuwa Februari 4, 1995 jijini Dar, es Salaam kwa nia ya kudanganya mshtakiwa huyo alighushi cheti cha ndoa chenye usajili namba 00040078.
Wakili Mwaitenda amedai kuwa mtuhumiwa huyo alifanya hivyo kwa nia ya kuonesha kuwa alifunga ndoa na Silvanus Mzeru (marehemu) Februari 4, 1995 katika kanisa Katoliki Mburahati wakati akijua si kweli kwa lengo la kujipatia mali za marehemu huyo.
Baada ya kusomewa shtaka hilo mawakili wanaomtetea mshtakiwa, Mtubika Godfrey na Juma Nyamgaruri waliiomba mahakama kumpatia dhamana mteja wao kwa sababu shtaka linalomkabili kwa mujibu wa sheria linadhaminika.
Mshtakiwa huyo baada ya kusomewa shtaka lake hilo, amekana na kudai Mzeru ni mumewe.
Upande wa mashtaka umedai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.