Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 5:35 am

NEWS: MWENGE WA UHURU KUTUA KWA PINDA KESHO

DODOMA: Wilaya ya Dodoma inatarajia kupokea mwenge wa uhuru wa mwaka huu wa 2017 siku ya kesho tarehe 25 juni ambapo unatarajiwa kupokelewa kutoka katika kituo cha veyula saa mbili kamili asubuhi ikiwa ni pamoja nakupitia miradi sita ikiwemo mradi wa ufunguzi wa wodi ya kina mama kwaajili ya kujifungulia katika zahanati ya Zuzu.

Akiongea na waandishi wa habari Mkuu wa wilaya ya Dododma Bi. Christina Mdeme amesema kuwa Mapokezi hayo yatapokelewa kutoka halmashauri ya mji wa kondoa na kufanyika shuguli ya utoaji wa ujumbe wa mwenge utakao tolewa na wakimbiza mwenge.

Bi. Mdeme ameongeza kuwa pia mwenge huo utaelekea kwa waziri mkuu msaafu Mizengo Pinda na lengo ni kuona shuguli mbalimbali za kilimo, mradi wa maji, ufugaji, mradi wa nyuki pamoja na shamba darasa hivyo Wananchi walio maeneo hayo wameomwa kushiriki kikamilifu ili kushuhudia shughuli hizo.

Sanjari na hayo amesema kuwa kwa mwaka huu eneo la mkesha litakuwakatika shule ya msingi Ipagala B ambapo kutafanyika mambo mbalimbali ikiwemo Joging, upimaji wa virusi kwa hiyari pamoja na onyesho la makomandoo.

Ujumbe wa mwenge wa mwaka huu ni shiriki kukuza uchumi wa viwanda kwa maendeleo ya nchi.