- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MWENGE WA UHURU KUTUA DODOMA
DODOMA: MWENGE wa uhuru umeingia leo Mkoani Dodoma ukitokea mkoani morogoro ambapo unatarajia kupitia jumla ya miradi 55 yenye thamani zaidi ya shilingi bilion 20.
Mwenge huo umepokelewa katika kata ya pandambii wilayani kongwa mkoani hapa akiongea wakati wa makabidhiano ya mwenge wa uhuru kaimu mkuu wa mkoa REHEMA NCHIMBI amesema serikali ya mkoa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wameweka mikakati ya kuhamasisha wawekezaji kuwekeza katika sekta ya viwanda ili kukuza uchumi wa wananchi wa mkoa huu.
Aidha katika mkoa wa Dodoma mwenge huo umeanza mbio zake wilayani kongwa ambapo mkuu wa wilaya hiyo DEO NDEJEMBI amekiri kuupokea na tayari kwa kufungua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo.
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Kongwa ambaye pia ni spika wa bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania mh.job ndugai yeye amesema ni vyema vijana wakafundishjwa maana ya mwenge ili uzidi kuenziwa.
Hata hivyo mwenge huo unatarajiwa kukimbizwa kwa muda wa siku 9 ndani ya Mkoa wa Dodoma na utapita katika wilaya zote saba za mkoa huu na kisha kukabidhiwa mkoani singida asubuhi ya juni 27 mwaka huu