- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MWENDESHA MASHTAKA AGOMA KUACHILIWA HURU GBAGBO
Jana Jumatano jioni Mwendesha mashitaka wa ICC Fatou Bensouda alikata rufaa dhidi ya uamuzi wa kuachiliwa huru siku moja baada ya ICC kumfutia mashataka Gbagbo na msaidizi wake Charles Ble Goude na kuamuru waachiliwe huru.
Mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa (ICC), Fatou Bensouda, ameomba Laurent Gbagbo na Charles Ble Goude kuendelea kuzuiliwa jela, wakati anaendelea kupata na kutathmini sababu zilizopelekea majaji kuamua kuachiliwa huru.
Fatou Bensouda ana hofu kwamba rais wa zamani wa Cote d'Ivoire na waziri wake wa zamani wanaweza kutoroka kabla ya kuendelea kwa kesi dhidi yao.
Alhamisi wiki hii majaji watano wa Mahakama ya Rufaa wanatarajia kuamua kama wanakubali au la rufaa ya mwendesha mashtaka iliyowasilishwa Jumatano jioni. Kama ombi la mwendesha mashitaka litakubaliwa Laurent Gbagbo na Charles Ble Goude wataendelea kuzuiliwa katika kituo jela la Scheveningen.
Kwa upande mwingine, ikiwa majaji watano watakataa rufaa na kuthibitisha uamuzi wa mahakama wa kuwafutia mashitaka, hatua itakayofauata ni kuachiliwa huru bila masharti.
Tayari nchi ya Ubelgiji imekubali kumpokea Laurent Gbagbo kama ataachiliwa huru.