Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 8:24 pm

NEWS: MWANZILISHI WA WEAKLEAKS AKAMATWA NA POLISI

Polisi nchini Uingereza imesema imemkamata Mwanzilishi wa Mtandao wa kufichua habari za Siri Duniani wa WikiLeaks Bw. Julian Assange katika Ubalozi wa Ecuador baada ya kukaa ndani ya Ubalozi huo kwa Takribani miaka 7

Bw. Assange amekuwa akiishi kama mkimbizi katika Ubalozi wa Ecuador nchini Uingereza kwa takribani miaka saba ili kuepuka kesi ya unyanyasaji wa kingono nchini Sweden.

Polisi wanasema kuwa wamemkamata Bw Assange baada ya kushindwa kujisalimisha mahakamani

Rais wa Ecuado Bw Lenin Moreno amesema kuwa alimuachia Bw. Assange baada ya kurudia kukiuka mkataba wa kimataifa

Wikileaks wali twitte kwamba Ecuador walikwenda kinyume kumuondolea Bw Assange hifadhi ya kisiasa.

Katibu mkuu wake wa Bw. Assange, Sajid Javid aliandika ujumbe kwenye Ukurasa wake wa Twiiter "naweza kudhibitisha Jualiana Assange kwasasa yupo kizuizini.

"napenda kushukuru Ecuador kwa ushirikiano na Polisi wa Uingereza kwa uweredi wao, hakuna mtu ambaye yupo juu ya sheria" alisema Bw. Sajid Javid