- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MWANDISHI WA DW KISWAHILI ALISHWA SUMU DODOMA
Dodoma. Mwandishi wa habari wa Idhaa ya Kiswahili ya sauti ya Ujerumani (DW) Deokaji Makomba amelazwa ghafla katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma nchini Tanzania Mara baada ya kudaiwa kulishwa sumu.
Deokaji alifikishwa hospitalini na polisi jana IJumaa Januari 3, 2020 saa 2 usiku akiwa hajitambui.
Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk Erenest Ibenzi amesema mwanzao alikuwa hana tarifa juu ya Mgonjwa huyo lakini Leo baada ya kufuatilia ndio akaelezwa kuna Mwandishi wa Habari ameletwa hapa akiwa hajitambui.
"nimeambiwa kwa sasa anaendelea vizuri, nimepanga kumuona Jioni muda huu nina vikao vingi kidogo" amesema Dkt Ibenzi
Polisi walimpata Deokaji baada ya basi la Ally's kumpeleka hapo akiwa hajitambui na waligundua wakati abiria wengine wakishuka ndipo wakamuona akiwa amelala hajitambui na hana kila kitu.
Deokaji amelzwa katika wodi namba nne kitanda namba saba licha ya wauguzi kusema kuwa anaendelea vizuri, lakini bado hana nguvu na nimtu wa kulala tu.
Akizungumza kwa tabu, anasema walitoka Mwanza kwa basi la kampuni ya Ally’s lakini alikuwa na fahamu hadi walipokaribia Bahi (Dodoma) ndipo hakujua kilichoendelea hadi alipojikuta yupo hospitalini.
"Wakati tunatoka Mwanza, nilikaa na mama mmoja lakini alishuka njiani ndipo akaja mwanaume aliyejitambulisha anafanya kazi uhamiaji, katikati ya Manyoni kuja Bahi, mwenzangu alikuwa anakula biskuits akanipa kama vipande viwili au vitatu na baada ya kula sikumbuki kama Bahi niliiona hadi nimestuka leo niko hospitali," anasema.