- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MWANDISHI KABENDERA BADO ANAENDELEA KUUMWA
Mwandishi wa habari za kiuchunguzi Erick Kabendera ameielezea Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumatano Septemba 18, 2019 kuwa jana amefanyiwa vipimo vya X- Ray na damu kwa mara ya kwanza katika Hospitali ya Rufaa ya Amana jijini Dar es salaam lakini hata hivyo bado anahisi maumivu makali katika mguu wake.
kabendera amesema hayo mbele ya Hakimu Mkazi mwandamizi Agustine Rwizile baada ya Wakili Mwandamizi wa Serikali Wankyo Saimon kueleza shauri lilikuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
"Nashukuru jana nilifanikiwa kwenda Hospitali ya Rufaa ya Amana na nilifanyiwa kipimo cha X Ray kwenye mgongo wangu na majibu yametoka," amesema Kabendera.
Kabendera amedai alikuchukuliwa kipimo cha damu na majibu yake bado hajapewa hivyo anaendelea kuvumilia ili majibu hayo yatoke aweze kuanza matibabu.
Pia ameieleza mahakama hiyo kuwa bado ana maumivu makali katika mguu wake jambo kubwa alilokuwa akisubiri ni kupatiwa vipimo ili aweze kuanza matibabu. Wakili wa utetezi, Jebra Kambole ameomba ahirisho hivyo shauri hilo litakapokuja wataieleza mahakama hiyo kuhusu majibu ya vipimo vya damu alivyochukuliwa.
Hakimu Rwezile baada ya kusikiliza maelezo hayo ameahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 1, 2019 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.
Kabendera ambaye ni mwandishi wa habari za ndani na nje ya Tanzania alifikishwa katika mahakama hiyo kwa mara ya kwanza, Agosti 5, 2019 akikabiliwa na mashtaka matatu ambayo ni kuongoza genge la uhalifu, kukwepa kodi na kutakatisha fedha zaidi ya Sh173.2 milioni.