- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MWANDISHI KABENDERA AMUOMBA RADHI RAIS MAGUFULI
Dar es Salaam. Mwandishi wa habari za uchunguzi nchini Tanzania, Erick Kabendera amemwomba radhi Rais wa Tanzania John Magufuli na Serikali ya nchi hiyo akiomba kusamehewa kama kuna makosa ameyafanya kama yeye.
Kabendera amesema hayo leo Jumanne Oktoba 1, 2019 jijini Dar es Salaam kupitia kwa wakili wake, Jebra Kambole.
Kambole amesema hayo muda mfupi baada ya kesi inayomkabili mwandishi huyo ya uhujumu uchumi na kutakatisha fedha Sh173.24 milioni kuahirishwa hadi Oktoba 11, 2019 kutokana na upelelezi kutokamilika.
“Sisi kama mawakili tunatoa ombi kwa Rais, kama Erick katika utendaji kazi wake kama kuna mahali alimkosea Rais au Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa niaba yake, familia yake, ndugu zake tumwombe radhi,” amesema Kambole
Katika kesi ya msingi, mshtakiwa anadaiwa katika siku tofauti kati ya Januari 2015 na Julai 2019 jijini Dar es Salaam, alitoa msaada katika genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia faida.
Katika shtaka la pili, inadaiwa siku na mahali hapo mshtakiwa bila kuwa na sababu za msingi kisheria alishindwa kulipa kodi ya Sh173.24 milioni ambayo ilitakiwa ilipwe kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Katika shtaka la utakatishaji fedha, kati ya Januari 2015 na Julai 2019 ndani ya jiji na mkoa wa Dar es Salaam mshtakiwa alijipatia kiasi hicho cha Sh173.2 milioni wakati akizipokea alijua kuwa fedha hizo ni mazao ya makosa tangulizi ya kukwepa kodi na kujihusisha na genge la uhalifu.