- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MWANASHERIA WA RAIS TRUMP AANIKA SIRI ZA TRUMP HADHARANI
mwanasheria wa zamani wa rais wa Marekani Donald Trump Bw. Michael Cohen, amemgeukia mteja wake wa zamani akidai aliratibu mipango ya siri kwa ujenzi wa jengo kubwa, hata wakati alikana kuhusika na biashara yeyote ya Urusi, huku akimuita Rais huyo kuwa "mbaguzi", "tapeli" na "muongo".
Michael Cohen, ametoa siri hizo mbele ya Bunge la Wawakili Jumatano ya jana , Februari 27.
Cohen ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu gerezani, hasa kwa kudanganya mbele ya bunge, alitoa nyaraka kadhaa ikiwa ni pamoja na nakala ya hundi mbili zilizosainiwa na Donald Trump baada ya kuchaguliwa kwake kuwa rais wa Marekani kwa kuwalipa wanawake wawili fedha kama kuwanyamanzisha juu ya uhusiano wao wa kimapenzi.
Katika taarifa yake ya ufunguzi,Michael Cohen alimkariri Donald Trump ambaye alimtumikia kwa zaidi ya muongo mmoja na kuelezea masikitiko yake kuona liweza kumtumikia. "Ninasikitikia siku niliyosema ndiyo kwa Bw Trump," Cohen amesema.
"Ninasikitikia msaada niliotoa na ambao unaendelea kumpa kibri. Najutia makosa yangu, na nimekubali hadharani kutowajibika kwangu na nakiri kuwa nimekosea katika Wilaya ya Kusini mwa New York.
Ameeleza pia kwamba Trump alifahamu kuhusu kufichuliwa kwa barua pepe zilizodukuliwa za chama cha Democrat na amemuita kiongozi huyo "mbaguzi", "tapeli" na "muongo".
Donald Trump amesema kuwa Michael Cohen anadanganya ili kupunguza kifungo chake gerezani."
Hata hivyo Cohen alikiri wazi kwamba Donald Trump hana biashara yoyote na Urusi.