- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MWANAMKE TAJIRI AFRIKA AKANUSHA MADAI YA UFISADI
Binti wa rais wa zamani wa Angola, Jose Eduardo dos Santos, Isabel mwenye Utajiri wa Dolla $3.7bilioni amekanusha vikali madai ya ufisadi baada ya mahakama mjini Luanda kuifunga akaunti yake ya benki. Isabel dos Santos anayeongoza kwa utajiri kwa wanawake Afrika amesema madai hayo dhidi yake yamechochewa kisiasa.
Isabel dos Santos anayeaminiwa kuwa mwanamke tajiri zaidi barani Afrika anachunguzwa kwa madai ya kufanya ubadhirifu wa fedha na kuzisababishia hasara kubwa kampuni za serikali ikiwa ni pamoja na kampuni kubwa ya mafuta ya taifa ‘Sonangol‘.
Baba yake Jose Eduardo dos Santos aliitawala Angola kwa miaka 38 na utawala wake unahusishwa na kukithiri kwa ufisadi na ubaguzi kwa madai kwamba aliyekuwa rais dos Santos aliwapendelea watu wa familia katika kuwapa vyeo serikalini hadi Rais Joao Lourenco alipochukua nafasi yake mnamo mwaka 2017.
Isabel, kama wengi wa wanafamilia ya dos Santos, aliondoka Angola, akidai alikabiliwa na vitisho vya kuuliwa baada ya baba yake kuondoka madarakani.
Aliteuliwa kuwa mkuu wa kampuni ya matuta ya taifa Sonangol mnamo mwaka 2016 lakini alitolewa kwenye wadhfa huo mwaka uliofuata wa 2017, katika hatua ya kwanza iliyofanywa na rais wa Angola Joao Lourenco ya kuwaondoa jamaa za dos Santos kutoka kwenye nyadhifa mbalimbali.