- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MWANAMKE AWA TAJIRI WATATU DUNIANI WAKIKE BAADA YA TALAKA
Binaadamu wa kwanza tajiri Duniani, ambaye ndie mmiliki wa mtandao wa Amazon Jeff Bezos, amekubali kumpa HISA mkewe MacKenzie ya 4% ya umiliki wa kampuni hiyo kubwa duniani baada ya kutalakiana itakayokuwa na thamani ya Dola za Kimarekani $35bn. Pesa hizo zitamfanya kuwa mwanamke wa tatu tajiri Duniani huku Jeff akisalia kuwa tajiri mkubwa duniani kwa mujibu wa jarida la Forbes.
Amazon iliyoasisiwa na Jeff Bezos huko Seattle mnamo 1994, mwaka mmoja baada ya wawili hao kuoana, na bi Bezos alikuwa mojawapo ya waajiriwa wa kwanza.
Jeff Bezos, mwenye umri wa miaka 55, na MacKenzie, wa miaka 48, walioana mnamo 1993 na wana watoto wanne.
Ujumbe wa Bi Bezo katika Twitter ni wa kwanza na wa kipekee tangu kujiunga na mtandao wa blogu mwezi huu. Katika ujunbe huo ameandika, "nimeshukuru kukamilisha talaka yangu na Jeff kwa ushirikiano wa pamoja".
Aliukamilisha ujumbe huo kwa kuandika: "Ni msaidizi, anayejituma, na mwenye mapenzi, na wakati maisha yetu yanafunguka katika siku za usoni, nafahamu kwamba nitaendelea kujifunza kutoka kwake."
Kabla ya makubaliano hayo Bezos alimiliki 16.3% ya kampuni ya Amazon. Ataendelea kushikilia 75% ya umiliki huo lakini Bi Bezos amewasilisha haki zake zote za maamuzi kwa mtalaka wake.
Anakabidhi pia hisa zake alizokuwa anamiliki katika gazeti la Washington Post na kampuni ya safari za anga za juu ya Bwana Bezos, Blue Original
Amazon ni kampuni ya mtandao inayotumika pakubwa duniani katika biashara ya mauzo.
Mwaka jana ilipata faida ya $232.8bn na imemsaidia Bwana Bezos na familia yake kukusanya utajiri wa $131bn, kwa mujibu wa jarida la Forbes.
Wote walituma ujumbe kumhusu mwenzake baada ya tangazo hilo la kufikiwa makubaliano ya talaka.