Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 2:35 pm

NEWS: MWANAMKE ACHUNGUZWA BAADA YA KUVAA SKETI FUPI

SAUDIA: Mamlaka nchini Saudia inamchunguza mwanamke mmoja aliyechapisha kanda yake ya video akiwa amevalia sketi fupi na tishet ilio wazi hadharani.

Mwanamke huyo ambaye ni mwanamitindo kwa jina Khulood alisambaza video hiyo akitembea katika ngome ya kihistoria ya Ushayqir.

Kanda hiyo ilizua hisia na mjadala mkali huku wengine wakitaka akamatwe kwa kuvunja sheria kali ya uvaaji wa mavazi nchini humo.

Raia wengine wa Saudia hatahivyo walimtetea mwanamke huyo wakimsifu kwa ujasiri wake.

Wanawake nchini Saudia ni sharti wavae nguo zisizowabana na ndefu kwa jina 'abaya' hadharani pamoja na kitambaa kichwani.

Pia hawaruhusiwi kuendesha magari na hutengwa na wanaume wasio kuwa na uhusiano wa kifamilia.

Katika video hiyo iliosambazwa katika mtandao wa Snapchat wikendi iliopita, Khulood anaonekana akitembea katika barabara isio na watu katika ngome hiyo ya historia ya Ushayqir yapata kilomita 155 kaskazini mwa mji mkuu wa Riyadh mkoani Najd.

Najd ni miongoni mwa maeneo ya kihafidhina nchini Suadia.

Ni eneo ambalo mwanzilishi wa Wahabi alizaliwa katika karne ya 18.

Video hiyo ilichukuliwa na watumiaji wa mtandao wa Twitter nchini humo ,ambapo kulikuwa na mjadali mkali kati ya wale wanaoamini Khulood angepaswa kuadhibiwa na wengine waliosisitiza kuwa anafaa kuwachwa kuvaa anachotaka.