- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MWANAHARAKATI ANAYEPINGA BREXIT AISHINDA SEREKALI YA UINGEREZA
Mwanaharakati anayepinga Uingereza kujiondoa Umoja wa Ulaya maarufu kama Brexit aliyeshinda shauri kuu dhidi ya serikali ya Uingereza Gina Miller amesema hii leo kwamba atarudi tena mahakamani iwapo waziri mkuu ajaye atajaribu kulazimisha Uingereza kujitoa kwenye umoja huo bila ya makubaliano.
Bi Miller ambaye pia ni mfanyabiashara amesema amewaagiza mawakili wake kumtahadharisha Boris Johnson wa chama cha Conservative anayetarajiwa kushika wadhifa wa uwaziri mkuu.
Bi Miller amesema itakuwa ni matumizi mabaya ya madaraka dhidi ya bunge iwapo atazuia sauti za wawakilishi waliochaguliwa na raia kufuatia matamshi ya Johnson kwamba Uingereza italazimika kuondoka Oktoba 31 kama ilivyopangwa.
Mwanaharakati huyo aliishinda kwa mara ya kwanza serikali mwaka 2017 kufuatia shauri lake la kuizuia kuhesabu siku za kuondoka kwenye Umoja huo kabla ya kura ya bunge.