Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 3:38 am

NEWS: MWANAFUNZI WA KIMAREKANI ALIYE ACHILIWA NA KOREA KUSINI AFARIKI DUNIA

MAREKANI : Otto Warmbier, mwanafunzi mwenye asili ya Marekani aliyekuwa na umri wa miaka ishirini na miwili, aliyerejeshwa nchini humo wiki iliyopita baada ya miezi kumi na mitano ya kushikiliwa nchini Korea Kaskazini, amefariki dunia siku sita tu baada ya kuachiliwa.

Familia yake imetoa lawama dhidi ya kifo hicho katika kile walichokiita unyanyasaji mkali dhidi ya Otto aliokuwa akikabiliana nao alipokuwa mikononi mwa maofisa usalama wa Korea Kaskazini .

Akiuelezea utawala wa Korea Kaskazini kama ni wa ukatili mkubwa , Rais wa Marekani Donald Trump amesema kwamba Warmbier alikabiliana na mazingira magumu akiwa nchini humo.

Akielezea hali ya kijana huyo amesema alikuwa katika hali ya kutojitambua pindi alipoachiliwa kutoka jela , na kuanzia hapo alilazwa hospitalini kwa matibabu zaidi karibu na nyumbani kwake Cincinnati.

Madaktari waliokuwa wakimtibia kijana huyo katika hospitali ya chuo kikuu cha tiba mjini humo wamesema kwamba kijana huyo alikuwa na majeraha makubwa ya kuumia neva.