- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MWANAFUNZI ALIYEONGOZA KITAIFA AFUNGUKA MBINU ALIZOTUMIA KUFAULU
Jana Baraza la mitihani la Taifa (NECTA) lilitangaza matokeo ya kidato cha kwanza ya mwaka 2018 ambapo Katibu mtendaji wa Baraza hilo Dr. Charles Msonde alimtangaza mwanafuzi Hope Mwaibanje mwenye umri wa miaka 18 kutoka shule ya ILBORU ndiye mwanafunzi aliyeshika nafasi ya kwanza kitaifa katika Mtihani wa Kidato cha nne mwaka jana.
Akizungumza Waandishi wa Habari jana akiwa jijini Mbeya baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, Mwaibanje alieleza jinsi ilivyokuwa ngumu kwake kuwa miongoni mwa wanafunzi 10 walioongoza kitaifa.
Alisema mara kwa mara walimu wao walikuwa wakiwaeleza kuwa, wakiweka juhudi katika masomo, watafanya vizuri kitaifa, ikizingatiwa shule yao (Ilboru) inasifika kwa kufanya vizuri na kutoa wanafunzi bora kitaifa mara kwa mara.
“Maneno haya ya walimu ndiyo yaliyonifikisha hapa nilipo, ingawa matarajio yangu hayakuwa haya, nilikuwa napambana niwe miongoni mwa wanafunzi 10 bora kitaifa lakini Mungu ameamua kuniinua zaidi namshukuru sana ” alisema
“Ratiba ya kuingia darasani ilikuwa inaanzia saa moja asubuhi hadi saa nane mchana, baada ya kutoka darasani kuanzia saa tisa alasiri hadi saa 12 jioni, nilikuwa najisomea mwenyewe. Baada ya hapo dini, tukimaliza kuanzia saa mbili usiku hadi saa sita nilikuwa najisomea. “Niseme ukweli kutoka moyoni, walimu wetu pia walikuwa karibu na wanafunzi, walikuwa wanatufuatilia hatua kwa hatua za ufaulu wetu.
Pia ninamshukuru Mungu kwa kuwa hakuniacha kila hatua. “Endapo mwanafunzi akiamua kuachana na mambo mengine na kufikiria yale tu ambayo yamewapeleka masomoni, kwanini basi mwanafunzi wa namna hii asifikie lengo lake la kupata ufaulu wa juu, ila wasimwache Mungu." Kinara huyo wa ufaulu alibainisha kuwa, kuanzia darasa la kwanza hadi la saba, akiwa Shule ya Msingi Lioto, Mbeya Mjini, alikuwa miongoni mwa wanafunzi watatu bora, lakini alikutana na wakali zaidi alipojiunga na Ilboru na changamoto kubwa kwake ilikuwa lugha ya Kiingereza.
“Si unajua, unapotoka shule za msingi za serikali, lugha ya Kiingereza huwa changamoto, lakini hili halikunifanya nirudi nyuma, mwaka wa kwanza ulikuwa na changamoto na ufaulu wangu haukuwa mzuri, lakini kuanzia kidato cha pili nilifanya vizuri," alisema.
Mwaibanje alisema alipata taarifa ya kufanya vizuri kwenye mtihani huo jana asubuhi baada ya rafiki yake, Allen Diadoni kumpigia simu kumjulisha kuwa ameongoza kitaifa. “Wakati huo nilikuwa nyumbani, sikuamini kwa sababu hayakuwa matarajio yangu, nikajua ananidanganya, lakini simu ziliendelea kupigwa za kupongezwa na baada ya muda nilihakikisha mwenyewe baada ya kuona matokeo yangu namshukuru Mungu," alisema.