Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 1:40 am

NEWS: MWALIMU MKUU KORTINI KWA KUMBAKA NA KUMPA UJAUZITO WANAFUZI

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Kigoma, imemsomea maelezo ya awali Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nyantole, Jason Rwekaza (42), ambaye anakabiliwa na makosa saba ya kumbaka na kumpa mimba mwanafunzi wake katika shule hiyo.

Mshtakiwa huyo alipandishwa kizimbani jana mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Frola Mtarania, na kusomewa maelezo ya awali na mwendesha Mashtaka wa Serikali, Clement Masua. Masua alidai kuwa mshtakiwa huyo alimbaka mwanafunzi mwenye umri wa miaka 17 kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Kaulananga (jina linahifadhiwa), na kuwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanafunzi huyo kuanzia Mei mwaka 2017.

Image result for Mahakama ya mkoa wa kigoma

Mwendesha mashtaka huyo alidai zaidi kuwa mshtakiwa aliwahi kufanya mapenzi na mwanafunzi huyo mara saba.

Alidai mshtakiwa alifanya mapenzi na mwanafunzi huyo mara ya tano Julai 10, mwaka 2018 maeneo ya Bigabilo Wilaya ya Kigoma na mara ya sita alifanya mapenzi na mwanafunzi huyo Februari 5, mwaka 2019 maeneo ya Kahabwa Manispaa ya Kigoma/Ujiji na mara ya saba mshtakiwa huyo alifanya mapenzi na mwanafunzi huyo Februari 10, mwaka 2019 maeneo ya Kahabwa Manispaa ya Kigoma/Ujiji kisha kupata ujauzito.

Alidai kuwa baada ya uongozi wa Shule ya Sekondari ya Kaulananga kulifahamu tukio hilo, ulitoa taarifa kwa wazazi wa mwanafunzi huyo. Kwamba Mei 31, mwaka 2019, tukio hilo liliripotiwa katika Kituo cha Polisi Kati na polisi walifanya mahojiano na mwanafunzi huyo, kisha alimtaja mshtakiwa kuwa ndiye aliyempatia ujauzito na baadaye mshtakiwa alikamatwa na alipohojiwa kwenye maelezo ya onyo alikana. Aliendelea kudai kuwa polisi walipomaliza upelelezi walimpeleka mshtakiwa huyo mahakamani.

Kwa mujibu wa Masua, upande wa mashtaka unatarajia kupeleka mashahidi 10 na vielelezo viwili, na kuomba mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kuanza kusikiliza kesi hiyo.

Upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili Thomas Msasa, uliomba mahakama kutoa amri ya kupima vinasaba (DNA), ili kuthibitisha kama mshtakiwa huyo ndiye aliyempa mwanafunzi huyo ujauzito. Baada ya upande wa utetezi kutoa ombi hilo, Hakimu alisema wataendelea kusikiliza makosa ya kubaka, na siku ya hukumu hatalihusisha kosa la mimba mpaka watakapopima vinasaba.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Agosti 26, mwaka huu, kwa ajili ya kuanza kusikiliza mashahidi. Mshtakiwa huyo huyo awali aliposomewa mashtaka dhidi yake alikana, na yuko nje kwa dhamana ya wadhamini wawili ambao walitoa barua ya utambulisho kutoka kwa ofisa mtendaji wa kata, na mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh. milioni tano kwa kila mdhamini.

#Nipashe