Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 5:32 pm

NEWS: MWAKYEMBE AWAPIGA MKWALA WANAOHOJI KUPOTEA KWA AZORY GWANDA

WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, ameoneshwa kushngazwa na wadau wa habari nchini wanaotaka kuelezwa mahali aliko, mwandishi wa gazeti la Mwananchi, Azory Gwanda aliyepitea kwa takribani mwaka na nusu sasa.

Akizungumza bungeni leo Jumanne, wakati wa mjadala wa bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha ujao wa fedha Dk. Mwakyembe, ametaka kupuuzwa kwa watu wanaotaka ripoti kamili ya kupotea kwa Azory.

Related image

Amesema mwandishi huyo aliyetekwa na watu wasiojulikana Novemba 21, 2017 amepotea katika mazingira ambayo Watanzania wengi wamepotea katika eneo hilo (Kibiti). Waziri huyo ametoa kauli hiyo leo Jumanne Aprili 23, bungeni jijini Dodoma wakati akijibu hoja za wabunge walizozitoa katika mjadala wa bajeti ya wizara hiyo mwaka wa fedha 2019/2020.

“Tunaongelea kesi ambayo ni dhaifu sana, mwandishi huyu amepotea eneo ambalo mamia ya Watanzania wengine wamepotea, hawauliziwi hao ila mmoja huyo ndio dhahabu.”

“Halafu inaulizwa Serikali ambayo imeshughulikiwa kiasi kikubwa na maofisa wa Serikali wengi wamekufa pale, najua mnawalisha Wazungu na wafadhili matango pori (uongo), hatujakosa chochote acha tushushwe madaraja, sisi tunaheshimu uhuru wetu kwanza,” amesema.

Mke wake, Anna Pinoni, alinukuliwa akisema, “…watu wapatao wanne, wakiwa kwenye gari aina ya Toyota Land Cruiser, yenye rangi nyeupe, walimchukua mume wake (Azory Gwanda), kutoka katikati ya mji huo, mahali ambapo hupendelea kukaa.

“Kwamba, aliporudi nyumbani alikuta vitu vimezagaa, ishara kuwa waliipekua nyumba yao.”

Mwandishi huyo mahiri wa habari, alikuwa akiishi na kufanyia shughuli zake katika mji mdogo wa Kibiti, mkoani Pwani.

Alikuwa mmoja wa waaandishi wa kwanza kabisa wa habari, kuripoti kwa kina, juu ya mfululizo wa mauwaji, yaliyokuwa yakitekelezwa katika eneo hilo.

Akitetea hoja yake ya kutaka wananchi kipuuza taarifa za kumtafuta mwandishi huyo, Dk. Mwakyembe amesema, kuna watu wengi wamepotea katika eneo hilo, wakiwemo vongozi wa serikali.

Ameapa kuwa “serikali itaendelea kuwadhibiti watu wanaokiuka utoaji wa maoni, kwa kuwa hakuna uhuru usiokuwa na mipaka.” Hakufafanua.