- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MWAKYEMBE AONYA WANASIASA WANAOZUSHA KUHUSU NDEGE YA BOMBARDIER NI MBOVU.
MBEYA: WATANZANIA wameaswa kuyapuuza maneno ya watu wachache hususani wanasiasa wanazusha kuwa ndege za serikali aina ya bombardier ni mbovu, kwa kuwa watu hao hawana utaalamu wa kutambua jambo hilo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe (pichani) alitoa rai hiyo katika mahojiano maalumu na waandishi wa habari akiwa katika chumba cha abiria kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe alipokuwa akijiandaa kusafiri kutoka Mbeya kwenda jijini Dar es Salaam kwa kutumia ndege ya Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) mapema wiki hii.
Dk Mwakyembe alisema wapo watu wamekuwa wakipiga kelele za uzushi kwamba serikali imenunua ndege mbovu, jambo ambalo siyo la kweli kwani mchakato wa upatikanaji wa ndege hizo ulianza muda mrefu ukiwashirikisha wataalamu mbalimbali kwa kuzingatia mazingira ya nchi pamoja na viwanja vilivyopo.
“Kuna watu wanasema ndege hizi ni mbovu sasa watuletee za kwao ambazo siyo mbovu. Kwanza hawana hata utaalamu wa kujua ndege nzima au mbovu pia wanachoangalia ni kutumia pangaboyi tofauti na zingine lakini ubora ni uleule,”.