- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MVUA KUBWA YAUA WATU ZAIDI YA 30 MJI MKUU WA CONGO KINSHASA
Raia zaidi 36 wamefariki dunia baada ya mvua kubwa kunyesha juzi Jumatatu usiku kuamkia jumanne katika mji mkuu wa DRC, Kinshasa, Naibu Gavana wa mji huo, Neron Mbungu amedhibitisha.
"Waziri wa Mambo ya Ndani wa mkoa ametoa taarifa ya vifo vya watu 36. Zoezi la kutafuta miili mingine ya watu waliofariki dunia au manusura linaendelea. Uharibifu wa vifaa na hasara kwa binadamu ni kubwa, "amesema Neron Mbungu, ambaye amebaini kwamba amezuru eneo lililoathirika.
Waathiriwa walipelekwa na maporomoko ya udongo. Madaraja mawili yameporomoka na barabara inayoelekea chuo kikuu katika Wilaya ya Lemba, imeharibika vibaya, ameongeza Naibu Gavana.
"Kuna mafuriko," amebaini Neron Mbungu, huku akisema kuwa "mtoto mmoja aliyeuawa na umeme" ni miongoni mwa waathiriwa.
Mamia ya watu walfariki dunia kutokana na mmomonyoko na maporomoko mapema mwezi Januari 2018 katika mji wa Kinshasa baada ya mvua kubwa kunyesha usiku kucha. Kinshasa mji wa tatu wenye watu wengi barani Afrika, una wakaazi milioni 10, ambao wengi wao wanaishi katika nyumba ambazo ni rahisi kuporomoka mvua inaponyesha.