- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MUSWADA WA SHERIA YA SERIKALI MTANDAO WAWASILISHWA BUNGENI.
BUNGENI: Serikali kupitia wizara ya Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, imewasilisha Bungeni muswada wa sheria ya serikali mtandao ili Bunge lilidhie na kuwa sheria hali itakayosaidia kuimarika kwa huduma mbalimbali serikalini.
Akiwasilisha bungeni leo kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo, Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughurikia Uwekezaji Angellah Kairuki, amesema endapo muswada utapitishwa kuwa sheria utasaidia serikali kuogeza udhibiti na kuboresha sheria mtandao hapa nchini.
Amesema kutaimarisha usimamizi wa ukasunyaji mapato ya serikali, matumizi ya rasilimali za HEHAMA katika taasisi za Umma kuboresha mazinngira ya biashara, mfumo wa leseni, kodi, benki, usimamizi wa ardhi, na utoaji hati za kusafiria.
Amesema utasaidia kuimarisha uwazi, ufanisi, uwajibikaji kupungua kwa gharama za uendeshaji, kudhibiti na kupunguza vitendo vya rushwa na utoaji huduma kwa umma kupitia TEHAMA.
Aidha amesema baadhi ya mambo yaliyozingatiwa ni pamoja na kuweka mfumo thabiti wa kisheria wa usimamizi uratibu, udhibiti na urekebu katika utekelezaji wa serikali mtandao kwa lengo la kuweka utaratibu.
Pia wakala ya serikali mtandao kuwa mamlaka itakayokuwa na majukumu ya usimamizi, uratibu, urekebu na utekelezaji wa sheria mtandao, kuweka utaratibu wa adhabu kwa watumishi au taasisi za serikali zisizozingatia miongozo inayotolewa, kuweka taratibu wa ushirikishwaji wa wadau katika utekelezaji wa sheria mtandao.