Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 3:23 pm

NEWS: MUSEVENI AYATAKA MATAIFA YA AFRIKA KUONDOA UKOMO WA MADARAKA

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ayataka mataifa ya Afrika yaondokane na sheria au kubadili katiba zao zinazowazuia viongozi wenye umri mkubwa na wale wamekwisha tawala kuwania urais katika nchi zao, kauli hii ya Museveni inakuja Mwezi mmoja baada ya Mahakama ya Juu nchini humo kuunga mkono hatua ya bunge kuondoa ukomo wa kuwania urais nchini Uganda.

Rais Yoweri Museveni wa Uganda anataka nchi za Afrika kubali kubadlisha katiba zao kuondoa vizuizi vyenye kuwakataza viongozi wenye umri mkubwa na wale ambao wametawala kwa muda mrefu kuwania urais.

Rais Yoweri Museveni amesema kwamba ukomo uliowekwa kwenye katiba kama vile ukomo kwa mihula na umri wa vinazuia Afrika kuwa na viongozi wazuri na wenye uzoefu.

Rais Museveni anajiandaa kuwania katika uchaguzi wa urais mwaka 2021 na akishinda, atakuwa mmoja wa viongozi wa Afrika wa waliotawala muda mrefu zaidi (miaka 40).

Bunge la Uganda limebadilisha katiba mara mbili na kumpa nafasi Museveni kuwani kwenye kiti cha urais . Mnamo mwaka 2005, bunge liliondoa ukomo wa mihula na mwaka 2017 likaondoa ukomo wa umri wa miaka 75 nakupa nafasi kuwania kwenye kiti cha urais mwaka 2021.

Rais Museveni alitoa mfano wa nchi ya Tunisia, kuthibitisha kwa nini watu wenye umri mkubwa wanapaswa kuendelea kuwa viongozi kwa nchi za Afrika

“Ukiwa na mtuu mzee mwenye umri wa miaka 75 kwa nini unasema aende wakati

anaweza kukusaidia? Kuna nchi inayoitwa Tunisia walifanya mageuzi lakini

walimtafuta mtu mwenye umri mkubwa wa miaka 88. Na huyo ndiye anawasaidia kwa sasa, ” amesema rais Museveni.

Mwanasiasa wa chama cha NRM Capt Mike Mukula ameunaga na hoja hiyo ya Museveni na kusema “nchi za Afrika zinapaswa kuzingatia nasaha ya rais Museveni”.

“Mambo ambayo Rais Museveni ametaja ni lazima tuanze kuyafikiria kama Waafrika sababu okiangalia nchi ambazo zimeendelea, hawana vizuizi kwenye katiba zao, ” amesema Mike Mukula.

Hata hivyo kauli hii ya Museveni imefutiliwa mbali na upinzani nchini Uganda, ukisema kuwa kauli hiyo inapotosha.

Kauli hiyo ni potofu kwa sababu itasababisha nchi nyingi Afrika kuongozwa na watu ambao wataendelea kusalia madarakani, na iwapo watafariki ,dunia kuna hatari familia zao kuendelea kutawala, jambo ambalo halikubaliki, “ amesema Gawaya Tegule, mwanasiasa wa upinzani ambeye pia ni mwanasheria.

Watataalam kuhusu mambo ya Utawala wanasema viongozi wakisalia muda mrefu madarakani wanapaswa kujihusisha na upendeleo, rushwa na ukiukwaji wa haki za binadamu