Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 4:01 am

News: Muhongo Auchana mradi wa umeme vijini [REA] kushindwa kulipa vibarua wake

Dodoma: Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospiter Muhongo, ameushukia mradi wa umeme vijijini (REA) kwa madai kuwa mradi huo ni kati ya miradi ambayo inalalamikiwa huku ukishindwa kulipa hata vibarua wake.

Prof. Muhongo ametoa kauli hiyo katika ofisi za nishati na madini mjini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mradi wa Umeme Vijijini REA Prof amelazimika kusema hayo kutokana na Mkuruugenzi wa REA,Gissima Nyamo-Hanga, kutoa takwimu ambazo zilionekana kuwa siyo sahii kwa kueleza kwa sasa asilimia 36 ya wakazi wanaoishi vijijini wanapata umeme.

Kwa taakwimu ambazo Prof Muhongo ameonesha kuziamini amesema kwa sasa wananchi waishio vijijini wenye fursa ya kutumia umeme ni asilimia 49.5.

“Kwa wananchi ambao walikuwa wanapata fursa ya kupata umeme mwaka 2007 ilikuwa asilimia 2 tu lakini kwa Desemba 30 mwaka jana wananchi waishio vijiji ambao wanapata umeme ni asilimia 49.5”alisema

Prof.Muhongo amesema jambo ambalo linasababisha REA kulalamikiwa ni kutokana na kukaa sana ofisini jambo ambalo linasababisha hata magari ya kuharibika mara kwa mara pale wanapokwenda kukagua miradi.

“Nimegundua kuwa REA wanapenda sana kukaa ofisini na ndiyo maana ninapokwenda katika kazi kwa vitendo utaona kuwa mara kwa mara nagari yao upata pancha, kuacha njia au kugonga mitii.

“Ndiyo maana nikagundua kuwa viongozi wanapenda kukaa ofisini na ndiyo maana hawana takwimu za uhakika ikiwa ni pamoja na kushindwa kutatua matatizo ambayo wananchi wanakumbana nayo ikiwa ni pamoja na vibarua kushindwa kulipwa fedha zao”alisema.

Prof. Muhongo pia amesema bodi hiyo lazima ihakikishe inawakagua wakandarasi wote ambao wameomba kazi na waliopewa kazi ili kubaini ubora wa viwango vya kazi.

“Nawaagiza bodi ya REA kuhakikisha wakandarasi wote wanakaguliwa na kutafuta historia zao na hata wale wakandarasi ambao ni kati ya nane ambao waliosimamishwa katiika mradi wa REA awamu ya pili kama wamepata tenda wachunguzwe hupya.

“Jambo lingine ninalowaagiza bodi ni kuhakikisha wakandarasi wadogo wasiajiliwe kutoka nje ya nchi badala yake wawe wakandarasi wa kutoka ndani ya nchi ili kuwafanya wakandarasi hao wadogo kujiongezea kipato” amesema Prof. Muhongo.

Hata hivyo ameiagiza bodi hiyo kutonunua vifaa kutoka njee ya nchi badala yake inunua vifaa vya ndani sambamba na kusimamia ubora.