November 26, 2024, 2:29 am
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MUGABE: WALIOWAUA WAZUNGU HAWATASHTAKIWA
ZIMBABWE: Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ameambia umati wakati wa sherehe za siku ya mashujaa kwenye mji mkuu wa Harare, kuwa watu ambao waliwaua wakulima wazungu wakati wa mabadiliko ya mifumo ya ardhi nchini humo hawatashtakiwa.
"Ndio tuna wale waliouwawa wakati walipinga. Hatuwezi kuwashtaki wale waliowaua. Ninauliza mbona tunawashtaki?" alisema Mugabe.
Wakati wa ukoloni, ardhi nzuri ilitengewa wazungu na mwaka 2000, bwana Mugabe aliongoza kutwaliwa kwa ardhi hiyo kutoka kwa wakulima 4000.
Rais Mugabe awali alikiri kuwa mifumo ya ardhi ya nchi hiyo ilifeli na mwaka 2015 alisema:
"Nafikiri mashamba tuliyowapa watu ni makubwa, hawawezi kuyasimami.
Kutaliwa ghafla mashamba kutoka kwa wakulima wazungu, inaonekana kuwa sababu kuu ya kuporomoka kwa uchumi wa Zimbabwe tangu mwaka 2000.
#BBCswahili