- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MUFTI ANAWAALIKA WANANCHI KWENYE KONGAMANO LA FAMILIA KIGABONI
Baraza kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) Chini ya Mufti wa Tanzania Abubakari Zubeir linawakaribisha Wananchi wote wa Dar es salaam na viunga vyake kwenye Kongamano la Kimalezi, Maadali na Amani litakalofanyika Siku ya Kesho Jumamosi ya Octoba 19, 2019 katika eneo la Kigamboni Jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Bakwata Wilaya Kigamboni leo Octoba 18, 2019 inasema kuwa leongo la Kongamano hilo ni Kujifunza namna ya kujenga Familia Bora yenye Upendo, Uchamungu na kufuata Miongozo ya Kidini, pia Kuombea Amani taifa la Tanzania.
Kongamano hilo linakusudiwa kufanyika kuanzia Asubuhi saa tatu mpaka jioni katika Uwaja wa Shababi karibu na shule ya Msingi ufukoni Kigamboni Jijini Da es salaam.
Kongamano hilo limeandaliwa na Ofisi ya Wilaya kigamboni linatarajiwa kuhudhuriwa na Sheikh Mkuu wa Tanzania Abubakar Zubeir, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Alhadi Mussa Salum, na Sheikh wa Wilaya ya Kigamboni Abdallah Idd, wengine ni Sheikh Othuman Maalim kutoka Zanzibar, Sheikh Zudin Jumanne kutoka Mombasa
Kongamano hilo linatarajiwa kuchagizwa na Zoezi la Kuchangia Damu, Mpira wa Miguu, na mashindano ya Qaswida.
Sheikh Abdallah Idd amesema kuwa wameamua kufanya kongamano hilo mara baada ya Kubaini kesi nyingi wanazoletewa Katika Ofisi ya Bakwata asilimia 80 kati ya kesi hizo ni migogoro ya kifamilia, kitu ambacho hakileti ustawi mzuri wa kifamilia na kimaadili nchini.
Amewataka wananchi wengi kujitokeza ili kujifunza kwa pamoja namna ya kukabiliana na changampto hizo na Kuliombea Taifa la Tanzania Amani.