Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 2:07 am

NEWS: MTUMISHI MBARONI KWA WIZI WA DAWA ZA ARV

Mtumishi mmoja katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora kitengo cha ugawaji dawa anayejulikana kwa jina la Francis Mlesa (33) anashikiliwa na Jeshi la Polisi Wilayani humo kwa tuhuma ya wizi wa a dawa zikiwemo za ARVs

Image result for hospitali ya igunga

Akizungumza na blog hii Ofisini kwake Ofisa Tarafa ya Igunga mjini Shadrack Kalekayo amesema tukio hilo lilitokea disemba 24 mwaka huu ambapo mtumishi huyo alishitukiwa na mlinzi aliyekuwa zamu majira ya sasa Mona na nusu usiku baada ya kumuona amefunga maboksi mawili kwenye baiskeli

Kalekayo amesema baada ya kukagua maboksi hayo ilibainika kuwa zilikuwemo dawa aina ya ARVs ila mtumishi huyo alifanikiwa kutoroka nazo baada ya mlinzi kuzidiwa na watu wanaopita getini hapo

Mlinzi aliyekuwa zamu siku hiyo Rushina ngeme Paulo alithibitisha kumkamata mtumishi huyo na dawa hizo akidai kuwa zimeisha muda wake na akidai kuwa alikuwa anaenda kuziteketeza ila mlinzi huyo alipoziangalia aliona kuwa zilikuwa hazijaisha muda wake

Amesema kuwa alitoa taarifa kwa uongozi wa Hospitali hiyo disemba 26,2019 na alifikishwa mbele ya uongozi ambapo alikiri kuiba dawa hizo huku akisema alizichukuwa kwa ajili ya kuziteketeza moto

Kwa upande wa watumishi wa Idara ya Afya hospitalini hapo ambao hawajataka majina yao yajulikane wamesema mtumishi huyo amekuwa akiwauzia Wafanyabiashara wa Ng'ombe kwa ajili ya kunenepesha mifugo yao

Kwa upande wake kamanda wa TAKUKURU Wilayani hapo Fransis Zuakuu amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo huku akisema alipigiwa simu na raia wema wakimjulisha kuwa kuna mtumishi ameiba dawa hospitalini na kutoroka nazo ambapo baada ya kumtafuta na kumkosa alimwagiza Mganga mkuu wa Wilaya hiyo Deus Ruha kumsaka ambapo disemba 26 walimpata na tayari yupo mahabusu katika kituo cha polisi Wilayani hapo

Aidha Nzuakuu ametoa wito kwa watumishi wa idara zote kufanya kazi kwa uadilifu na kujiepusha na vitendo kama hivyo kwani Serikali haitafumbia macho mtumishi Yeyote atakayebainika na vitendo kama hivyo vya wizi wa dawa za Serikali

Hata hivyo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Tabora ACP Barnabas Mwakalukwa alipoulizwa juu ya tukio hilo amethibitisha kushikiliwa kwa Francis Malesa huku akisema kwa sasa hawezi kuzungumzia suala lolote kwani bado wanaendelea kumhoji ili kubaini thamani ya dawa zilizoibwa.