Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 3:39 pm

NEWS: MTOTO WA RAIS ZUMA AKANA KUTOA RUSHWA YA BIL 90

Gazeti la Daily Monitor limeripoti kuwa Mtoto pendwa wa aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, Duduzane Zume amekana vikali tuhuma zinazomkabili kuwa alitaka kumpa rushwa ya zaidi ya Tsh. Bilioni 92 kwa aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha wa kipindi hicho Bw. Mcebisi Jonas.

Duduzane Zuma (35) akiwa mbele ya Mahakama ili kujibu tuhuma za kuwa kiunganishi kikuu cha mnyororo wa rushwa uliotengenezwa na Baba yake Rais Zuma

Jonas aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha amesema kuwa Ajay Gupta kutoka familia ya wafanyabiashara wakubwa nchini humo alikuwepo katika kikao hicho kilichoandaliwa na Duduzane

Duduzane amekana kuwa katika kikao hicho hakukuwa na ahadi ya fedha wala Ajay Gupta hakuwepo eneo hilo

Naibu Waziri huyo amesema kuwa alipewa ofa ya dola $40milioni sawa na zaidi ya Tsh Bilioni 90 kutoka kwa miongoni mwa kaka wa Gupta anaitwa Ajay na aliahidiwa kupandishwa cheo kuwa Waziri kamili lakini awezeshe biashara yao kwenda vizuri.

Pia alipewa onyo iwapo hatapokea ofa hiyo atauwawa.