- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MTOTO WA RAIS WA MSUMBIJI ANASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA RUSHWA
Mtoto wa kwanza wa rais wa zamani wa Msumbiji Armando Guebuza Bw. Ndambi Guebuza,anazuiliwa na vyombo vya usalama nchini Humo kwa tuhuma za kuunda mtandao wa kula deni la taifa lilofichwa la nchi hiyo.
Deni hilo lilichukuliwa baaada ya serekali ya nchi hiyo Kukopa zaidi ya dola za kimarekani bilioni $2 kutoka katika makampuni ya Umma
Ndambi Guebuza alikamatwa akiwa nyumbani kwake katika uchunguzi kuhusu mtandao wa rushwa aliotumia kwa kuchukuwa "deni lililofichwa" la taifa hilo la kusini mwa Afrika.
Kashfa hiyo ya rushwa ilianza miaka kumi iliyopita. Serikali ya Maputo imekuwa ikichukuwa mikopo kupitia makampuni ya umma kwa zaidi ya dola Bilioni mbili.
Kiwango hiki ni kikubwa ukitalinganisha na pato la Taifa la Msumbiji. Pato hilo kwa sasa linakaribia dola Bilioni 16. Mikopo hutolewa na Bunge pamoja na wakopaji wa kimataifa.
Fedha hizi zinawezesha kununua meli, vyombo mbalimbali vya kusafiria, lakini pia meli za kijeshi, vifaa ambavyo kwa sehemu mmoja vimetengenezwa nchini Ufaransa.
Lakini siri hiyo haijafichwa kwa muda mrefu. Mnamo mwaka 2016, "deni hilo lililofichwa" lilidhihirika siku moja na wakati huo uchumi wa Msumbiji ulijikuta pabaya.
Nchi hiyo inakabiliwa na mdororo wa kifedha tangu ilipopata uhuru wake. Wengi wa wafadhili wamesitisha misaada yao na serikali ya Maputo italazimika kusitisha zoezi la kulipa madeni yake. Kwa leo sasa, serikali inajaribu kuomba tena mazungumzo na wafadhili wake.
Mashirika yasiyo ya kiserikali yanakataa serikali kulipa "madeni yaliyofichwa" kutokana na kuwa bado kuna mashaka makubwa kuhusu matumizi ya fedha hizo.