- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MTOTO WA MKUU WA MAJESHI NCHINI NDIE ALIYEFARIKI AJALI YA NDEGE
Dar es Salaam. Mtoto wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Tanzania (CDF), Jenerali Venance Mabeyo ni miongoni mwa watu wawili waliofariki katika ajali ya ndege ya Kampuni ya Auric iliyotokea leo asubuhi Jumatatu Septemba 23, 2019.
Nelson Mabeyo ndio alikuwa rubani wa ndege hiyo iliyoanguka katika uwanja mdogo wa ndege wa Seronera uliopo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti nchini Tanzania.
Ndege hiyo ilianguka majira ya saa 1:30 asubuhi wakati ikipaa katika uwanja huo kwenda mkoani Arusha.
Habari za uhakika kutoka mamlaka ya viwanja wa ndege imeeleza kuwa Nelson aliondoka na ndege hiyo jana katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam.
Habari za uhakika kutoka mamlaka ya viwanja wa ndege imeeleza kuwa Nelson aliondoka na ndege hiyo jana katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam.
Akizungumza na gazeti la Mwananchi katika uwanja wa ndege wa Soronera, Msimamizi wa Kampuni ya Auric, Peter Kimaro amesema Nelson amefariki katika ajali hiyo akiwa na Nelson Orutu ambaye ni rubani mwanafunzi.
“Baada ya kuhakiki na kuona ndege iko sawa na kuruhusiwa kuruka kwenda Gurument kuwachukua wageni kuwapeleka KIA (Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro), walipoingia na kuondoka na mimi nikajua wako sawa,” amesema.
Amesema baada ya kuona ndege imeshika mwendo kisha ikapaa kidogo, badala ya kunyooka juu ikakata kona, “na mimi nikashangaa kuona vile kisha ikagonga choo cha uwanjani na kuanguka na wote walifia ndani ya ndege.”
Amesema jeshi la zima moto na uokoaji waliwahi kuzima moto na miili imehifadhiwa katika Zahanati ya Soronera ikisubiri utaratibu mwingine.