- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MTOTO WA MBOWE AAMBUKIZWA CORONA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema kuwa Mwenyekiti wa chama cha Upinzani CHEDEMA Freeman Mbowe amesitisha mikutano ya hadhara kama alivyokuwa ameahidi mara baada ya mtoto wake kukutwa na maambukizi ya virusi vya Corona.
Kauli hiyo Makonda ameitoa asubuhi ya leo Machi 24, 2020 akiwa stendi ya mabasi ya Ubungo akizungumza na wasafiri wa kwenda mikoani ili wachukue tahadhari kuhusu virusi hatari vya corona.
"Tusikubali kupokea ushauri wa wanasiasa uchwara kama akina Mbowe, sikilizeni Ushauri wa Viongozi wenu"
"Watu kama hawa asingeugua mtu wa familia yake, aliyetoka njee kaja na huo ogonjwa mngeingizwa kwenye mamikutano, angeleta mvutano kati ya Serekali na Wanasiasa" na Dunia ingeanza kuona kuwa serekali ya Tanzania haina Demokrasia" amesem Makonda
Aidha RC Makonda tayari amewaelekeza Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanatenga maeneo maalumu ya kuwahifadhi wageni wanaotoka nje ya Nchi (karantini) ili wawe chini ya uangalizi kwa muda wa siku 14, huku akiwahimiza Wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya corona.
"Hotel tunazotenga hatutozitangaza maana tunafahamiana, ni kama vile tungewaambia Watanzania wote wakae ndani kuna Watu wangetoka kuchungulia tungejikuta wote tupo mitaani, Wenyeviti wa mitaa wahakikishe wanawatambua wageni kwenye maeneo yao