- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MTATURU ATOA MSAADA WA SHILINGI MILIONI 11.2 KATIKA SEKTA YA ELIMU.
IKUNGI SINGIDA: Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki Miraji Mtaturu amekabidhi kompyuta 5,printer 1,na panel 3 za umeme jua vyenye thamani ya shilingi milioni 11.2 kwa shule ya sekondari ya Dokta Ally Mohamed Shein iliyopo jimboni humo.
Akikabidhi vifaa hivyo shuleni hapo,Mtaturu amesema amechukua uamuzi huo kama hatua ya kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano katika kuimarisha utoaji wa elimu bila ya malipo ikiwemo kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.
“Vifaa hivi nimeleta kwenu kama nilivyoahidi na lengo langu ni kuzifikia shule zote zilizopo jimboni humo ambazo hazina huduma ya umeme,namuomba Mwenyezi Mungu aniwezeshe nitimize dhamira niliyonayo,vifaa hivi vitakuwa chachu kwenu wanafunzi kujifunza teknolojia ya habari na mawasiliano kwa urahisi,lakini pia itasaidia kuongeza ufaulu wa wanafunzi,
Amesema panel za umeme jua alizopeleka zina uwezo wa kuwasha umeme shule nzima na kusisitiza kuwa ataendelea kuunga mkono juhudi za serikali katikak uhakikisha sekta ya elimu inaboreshwa jimboni humo.
“Nimeleta salamu za Rais wetu Dkt John Magufuli anawasalimia na kuwatakia kila la kheri,nimeleta pia salamu za naibu waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Atashasta Nditiye ambaye aliahidi kuwaletea printer moja na ametekeleza ahadi hiyo,”alisema Mtaturu.
Kwa upande wake Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)wilaya ya Ikungi Pius Sankha amemshukuru mbunge kwa kuitekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa vitendo na kusema kama chama wanaendelea kufuatilia utendaji wake jimboni na wanaridhishwa sana.
"Tangu uapishwe septemba 3 mwaka jana umefanya kazi nzuri na kutukuka,unasaidia chama chetu katika utekelezaji wa Ilani,umekuwa nembo nzuri ya chama chetu, na tumeendelea kufuatilia utendaji wako jimboni na tunaridhishwa sana,"alisema Sankha.
Mbali na kutoa misaada hiyo Mbunge Mtaturu pia ametimiza ahadi yake ya kutoa kiasi cha shilingi laki moja kwa mwanafunzi pekee Yassin Itambu aliyepata daraja la kwanza ambaye pia amejitolea kugharamia elimu yake ya kidato cha tano na cha sita na shilingi 160,000 kwa wanafunzi 8 waliopata daraja la pili ambao kila mmoja atapata 20,000 kama alivyowahi kuwaahidi.